RPC Shanna-Asisitiza madereva wawili kwenye mabasi ya mikoani yaendayo masafa marefu - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka

Habari za Hivi Punde

Tangaza Hapa +255755300337

Post Top Ad

Post Top Ad


Friday, 5 January 2018

RPC Shanna-Asisitiza madereva wawili kwenye mabasi ya mikoani yaendayo masafa marefu

 Madereva wa mabasi ya abiria yaendayo mkoani yakikaguliwa katika stand kuu ya mabasi Mailmoja  kwenye misako mbalimbali ya makosa ya usalama barabarani inayoendelea mkoani .
Pwani.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani (ACP)Jonathan Shanna akizungumza jambo na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na masuala ya usalama barabarani Mkoani hapo.
(Picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

JESHI la polisi mkoani Pwani ,limetoa agizo kwa wamiliki wa vyombo vya moto ambavyo vinasafirisha abiria kwenda mikoa ya mbali ikiwemo yale yanayokwenda zaidi ya masaa nane kuzingatia uwepo wa madereva wawili .

Aidha limekemea madereva wanaoamka na vileo kichwani kuacha tabia hiyo kwani wapo baadhi ya madereva ambao udamka na vileo na kuendelea na safari suala ambalo ni hatari kwa abiria na usalama wao.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha mkoani Pwani,kamanda wa polisi mkoani hapo,(ACP)Jonathan Shanna alisisitiza kuwa agizo hilo lilikuwa sio la wakati wa sikukuu pekee.

Alisema ni zoezi endelevu na wanaendelea na misako mbalimbali ya makosa ya usalama barabarani bila kikomo.

Kamanda Shanna alisema ,magari yatakayobainika kutokuwa na madereva wawili hayataruhusiwa kuendelea na safari zao.

Katika hatua nyingine,aliwataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na wale wenye tabia za kutumia vileo kisha kuendesha vyombo vya moto kuacha mara moja .

Kamanda huyo alisema,madereva wengi wamekuwa wakijiwekea kuwa maagizo na misako inayohusiana na masuala ya usalama barabarani ni ya mpito lakini anatoa salamu ,kuwa jeshi hilo halipokufurahisha mtu ila inafanya kazi zake kwa misimamo.

Kamanda Shanna,aliwahakikishia madereva wa aina hiyo kwamba hawataweza kuingia mkoani humo na kupita pasipo kukamatwa na askari wao mahiri wa kikosi cha usala barabarani ambao wapo kila mahali.

Alitoa wito kwa madereva wasio na uzoefu kutokwenda safari za mbali na kuwataka wamiliki kuacha njia za mkato wakihitaji madereva wa kwenda safari za mbali watafute madereva wenye uzoefu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Tangaza Hapa +255755300337