Header Ads


Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson kupitia Taasisi ya Tulia (Tulia Trust Fund) akabidhi TV sita (6) kwa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete JKCI

 Naibu Spika wa Bunge Mhe.  Dkt.  Tulia Ackson akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Fedha Agnes Kuhenga Televisheni moja kati ya nne zilizotolewa na Taasisi ya Tulia (Tulia Trust Fund) kwa ajili ya watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Jumla ya TV sita zimetolewa na Tulia Trust ambazo zimefungwa  katika wodi na kliniki za watoto.
 Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Delila Kimambo akimweleza  Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt.  Tulia Ackson maendeleo ya afya za pacha walioungana Maria na Consolata waliolazwa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya Matibabu.
 Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt.  Tulia Ackson akiwajulia hali pacha walioungana Maria na Consolata waliolazwa  katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)kwa ajili ya Matibabu.
 Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu.  Mhe. Dkt. Tulia kupitia Taasisi ya Tulia (Tulia Trust Fund) ametoa TV sita kwa JKCI ambazo zimefungwa  katika wodi na kliniki za watoto.
Picha na JKCI
.............
Na Mwandishi wetu
11/01/2018 Naibu Spika wa Bunge Mhe.Dkt. Tulia Ackson amekabidhi Televisheni nne ambazo zimefungwa kwenye wodi za watoto na kliniki katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Mhe. Dkt. Tulia alikabidhi TV hizo leo kupitia Taasisi ya Tulia Trust  imepokea Televisheni  nne kutoka Taasisi ya Tulia Trust  spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akabidhi msaada wa  televisheni sita kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKC I) kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuka jijini Dar es Salaama Dkt. Tulia alisema wamekabidhi jumla ya televisheni sita kwa JKCI zinazogharimu  jumla ya Sh million sita.
“Niliguswa kutoa msaada huu nilipokuja kwa mara ya kwanza kumtembelea mtoto ambaye taasisi ya Tulia Trust tulimlipia gharama za matibabu.
Naibu spika aliongeza kuwa Taasisi yake inajihusisha na uboreshaji wa huduma za kijamii kama elimu, afya na miundo mbinu
“Sisi tunajishughulisha na uboreshaji wa huduma za kijamii kama afya na eimu, huwa tunapokea maombi  ya kusaidia kutoka kwa watu mbalimbali wenye uhitaji na wengine huwa  tunapoenda na kukuta tatizo kama nilivyokuja hapa kwa mara ya kwanza, kisha  tunashirikisha wadau na kujua jinsi ya kutatua,” alisema.
Dk. Tulia aliongeza kuwa Taasisi ya Tulia Trust wanakusudia kuzifikia hospitali nyingi zaidi kwanzia za mikoa ,Tarafa na hospital zinazotoa huduma kwa watoto kutokana na muitikioa wa wadau wanaofanya nao kazi.
 “Tunakusudia kuzifikia Hospital za Rufaa, Mikoa na nyingine zinazotoa huduma za afya kwa watoto kwa kuzipatia misaada mbalimbali kutokana na uhitaji kama kujenga vyumba vya upsuaji, kugawa mifuko ya sementi, mabati, vitanda na vifaa tiba” alisema.
Kwa upande wa  Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo kwa Watoto  kutoka Taasisi ya Moyo ya Moyo Jakaya Kikwete( JKCI)  Sulende Kubhoja aliishukuru taasisi hiyo, kwa kuwasaidia kupata televisheni hizo.
“Tunashukuru kwa msaada huu wa televisheni kwani unatoa upweke kwa watoto waliolazwa hapa, kwa wengine wenye kujaaliwa uwezo tunawakaribisha kusaidia Taasisi yetu” alisema.
Wakati huo huo  Naibu spika Dk.Tulia Ackson alitumia muda huo huo kuwatembelea pacha walioungana wanaopatiwa matibabu katika Taasisi hiyo.
 Dk. Tulia aliwapa pole kwa kuugua na kuwapongeza kwa kufanya vema katika masomo yao hatua ambayo imewawezesha kujiunga na Chuo Kikuu Ruaha.
“Nimekuwa nikipata taarifa zenu za kuugua poleni sana, sikupata muda wa kuonana na nyie ni chukue fursa hii pia kuwapongeza kwa kufanya vizuri kwenye masomo yenu” alisema.

No comments

Powered by Blogger.