Kamati ya maadili yaagizwa kumuhoji Mhe. Ole Sendeka - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka

Habari za Hivi Punde

Tangaza Hapa +255755300337

Post Top Ad

Post Top Ad


Tuesday, 9 January 2018

Kamati ya maadili yaagizwa kumuhoji Mhe. Ole Sendeka

 Mheshimiwa Job Ndugai (Mb) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameielekeza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kukutana ili kuchunguza na kujadili kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mheshimiwa Christopher Ole Sendeka, inayodhalilisha Bunge.

Mheshimiwa Spika amechukua hatua hiyo kufuatia kauli zilizonukuliwa katika mitandao ya kijamii kwa lugha za kimasai, kiswahili na kiiengereza, zikiashiria kejeli na dharau kwa Bunge na hivyo ameelekeza kuwa wakati wa kuchunguza suala hilo Kamati imuite na kumuhoji ili kubaini ukweli na dhamira ya kauli hizo na kutoa mapendekezo kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa na Bunge.

  Imetolewa na: Ofisi ya Spika
S.L.P. 941
DODOMA

09 Januari 2018

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Tangaza Hapa +255755300337