Header Ads


India kuendelea kuwajengea uwezo Watanzania

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb), katikati, akiwa katika kikao na balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya, wa pili kutoka kushoto.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb), akiwa katika kikao na balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya, wa pili kutoka kushoto.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni (mstaafu) Mhe. George Mkuchika (Mb) ameiomba Serikali ya India kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa umma nchini.

Mhe. Mkuchika amesema hayo leo katika kikao na Balozi wa India nchini Mhe. Sandeep Arya  ambaye ameahidi nchi yake kuendelea kutoa ufadhili katika fani mbalimbali kwa Watanzania.

“Watumishi kujengewa uwezo katika maeneo yanayohusu  TEHAMA, Afya na Viwanda yatasaidia sana nchi yetu” Mhe. Mkuchika amesema mpango wa maendeleo wa Taifa wa 2025 unatilia mkazo viwanda ili kuleta mabadiliko ya uchumi na jamii.

Balozi Sandeep Arya kwa upande wake amesema nchi yake imepanga kwa siku za usoni kuendesha warsha na mafunzo kwa njia ya kieletroniki (e-corses) ambapo katika eneo la Afya amesema ili kujenga uwezo zaidi utafanyika utaratibu wa kubadilishana wataalam wa afya kati ya nchi yake na Tanzania.

“Tunapanga pia kuleta watalaam na kutoa mafunzo hapa Tanzania” Balozi Arya amesema na kuongeza kwa mwaka huu 2018 wameongeza mafunzo kuhusu vita dhidi ya madawa ya kulevya ikiwamo matumizi na usafirishaji wake.

Imetolewa na

Florence Lawrence
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano-UTUMISHI

05.01.2018

No comments

Powered by Blogger.