CCM Tabora Yawataka Wanafunzi Kutoona Upandaji Miti ni Adhabu Bali ni Akiba Kwao. - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka

Habari za Hivi Punde

Tangaza Hapa +255755300337

Post Top Ad

Post Top Ad


Wednesday, 10 January 2018

CCM Tabora Yawataka Wanafunzi Kutoona Upandaji Miti ni Adhabu Bali ni Akiba Kwao.


NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Tabora kimewataka wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari kujenga tabia na utamaduni wa kupanda miti ya matunda na kivuli kwa ajili ya manufaa yao ya siku za usoni.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Igunga na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Hassani Wakasuvi wakati aliposhiriki uzinduzi wa upandaji miti kando kando ya barabara kuuu kutoka Tabora kuelekea Singida uliozinduliwa na Mkuu wa Mkoa huo Aggrey Mwanri kwa ajili ya wanafunzi hao.

Alisema kuwa wanafunzi wasione kitendo cha upandaji miti kinachoongozwa na viongozi wa kuanzia ngazi ya kitaifa kwenda mikoani hadi ngazi za chini kuwa ni adhabu bali kina manufaa na muhimu katika maisha yao ya baadaye.

Wakasuvi alisema kuwa ni vema wakafanya utaratibu huo kuwa wakudumu kwa kupanda miti mbalimbali ikiwemo ya matunda kwa wingi katika maeneo ya mashule na majumbani ili wapate chakula na kivuli.

“Nawaomba wanafunzi achene masuala ya ku-chat katika someni sana na  pandeni miti kwa wingi ili mpate kivuli na matunda …na kazi hii msiione kama ni adhabu bali ni akiba mnayojiwekea kwa ajili yenu na vizazi vyenu” alisema Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Tabora.

Aidha Mwenyekiti huyo alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa alivyojitokea katika kuhakikisha kuwa miti inapandwa kwa wingi katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika barabara kuu kwa ajili ya kutaka kuigeuza Tabora kuwa ya kijani na kurudisha uoto wa asili wa eneo hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora alisema kuwa wamekusudia kuhaklikisha barabara zote zinaingia mkoani humo na za ndani zinapandwa miti kuanzia mikoa wanayopakana nayo kwa njia ya mstari ili kuweka madhari mazuri na kuvutia watalii.

Alisema kuwa wanataka kuhakikisha mgeni anapoingia katika Mkoa huo anakaribishwa na miti iliyopandwa kwa wingi katika mistari iliyonyoka.

Mwanri alisema kuwa zoezi linafanywa na wakazi wote wa Mkoa wa Tabora kuanzia mashule hadi majumbani ili kujenga utamaduni wa eneo hilo kupenda miti na kuacha tabia ya kukata ovyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Tangaza Hapa +255755300337