Suma JKT Guard yatakiwa kutumia mbinu na teknolojia ya kisasa katika ulinzi - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka

Habari za Hivi Punde

Tangaza Hapa +255755300337

Post Top Ad

Post Top Ad


Tuesday, 12 December 2017

Suma JKT Guard yatakiwa kutumia mbinu na teknolojia ya kisasa katika ulinzi

 Wahitimu wa mafunzo ya kampuni ya ulinzi ya Suma Jkt wakiwa kwenye kufunga mafunzo ya kampuni ya ulinzi ya Suma Jkt kwenye kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha 832 Kj cha Ruvu Mlandizi - Kibaha.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
 Mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi ya Suma Jkt Meja Alfred Mwaijande  akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kampuni ya ulinzi ya Suma Jkt kwenye kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha 832 Kj cha Ruvu Mlandizi - Kibaha.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
 Mwakilishi wa mkurugenzi wa Suma Jkt Luteni Kanali Peter Lushika ,akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kampuni ya ulinzi ya Suma Jkt kwenye kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha 832 Kj cha Ruvu Mlandizi - Kibaha.(picha na Mwamvua Mwinyi)
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo ,akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kampuni ya ulinzi ya Suma Jkt kwenye kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha 832 Kj cha Ruvu Mlandizi - Kibaha.(Picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo ,ameitaka kampuni ya Ulinzi ya Suma JKT Guard Ltd,kutumia mbinu na teknolojia ya kisasa katika ulinzi na kuachana na mbinu za kizamani.

Aidha ameimwagia sifa kwa kubuni kampuni hiyo ya ulinzi  ambayo inatoa ajira kwa vijana walio wengi ambao wanakosa ajira jeshini.

Mhandisi Ndikilo,aliyasema hayo ,wilayani Kibaha wakati wa kufunga mafunzo ya kampuni hiyo ya ulinzi ya Suma Jkt kwenye kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha 832 Kj cha Ruvu Mlandizi - Kibaha.

Mhandisi Ndikilo aliwataka watumieni teknolojia zinazoenda na wakati wa kisasa katika ulinzi kwani baadhi ya wahalifu wamekuwa wakitumia na kuendana na teknolojia kwenye uhalifu.

Hata hivyo alisema ,kampuni hiyo imeisaidia serikali katika kutoa ajira kwa vijana ambao wamekuwa wakihangaika kutafuta ajira.

"Tunaishukuru Suma Jkt Guard kwa kuanzisha kampuni ya ulinzi ambayo imewachukua vijana waliokosa nafasi za jeshi ambao wangeingia mitaani ingeleta shida kubwa kwani wengine wangeweza kuwa wahalifu,"

"Wangekuwa wavuta bangi,wangekaa vijiweni ,lakini kampuni hii imekuwa msaada mkubwa na kuwapa fursa vijana wazalendo wa kitanzania" alisema mhandisi Ndikilo.

Alieleza vijana sasa wamepata njia mbadala ya kuwapatia vijana ajira za uhakika mara wanapomaliza mafunzo yao ya kijeshi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi ya Suma Jkt Meja Alfred Mwaijande alisema , mafunzo hayo ya miezi minne wahitimu wamejifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi ya silaha na uadilifu katika kazi.

Mwaijande alielezea ,kampuni hiyo inawaandaa walinzi ambao ni waadilifu na wanatumia mafunzo yao kwa weledi mkubwa.

Alisema vijana waliopata mafunzo hayo wanapata ajira kwenye kampuni hiyo na watasambazwa nchi nzima na kuwataka wajiepushe na tamaa.

Nae mwakilishi wa mkurugenzi wa Suma Jkt Luteni Kanali Peter Lushika ,alisema wataanzisha chuo cha mafunzo hayo badala ya kutokuwa na sehemu maalumu ya kuwapatia mafunzo .

Lushika alisema , tayari wameshapata kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa chuo huko Kihonda mkoani Morogoro.

Akisoma risala ya wahitimu Deogratias Charles ,alisema kuwa wamepata mafanikio makubwa kwa kuweza kujifunza mbinu mbalimbali za usalama,utimamu,nidhamu utii na uhodari.

Charles alisema kwamba,changamoto iliyopo ni pamoja na mavazi hasa yale ambayo yanaendana na wakati hasa kipindi cha mvua.

Jumla ya wahitimu 529 walihitimu mafunzo hayo yaliyoanza Agosti makao makuu miezi mitatu na baadaye kuja kumalizia Ruvu mwezi mmoja.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Tangaza Hapa +255755300337