Mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kujifanya daktari daktari feki - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka

Habari za Hivi Punde

Tangaza Hapa +255755300337

Post Top Ad

Post Top Ad


Tuesday, 19 December 2017

Mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kujifanya daktari daktari feki

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 17.12.201
KWAMBA TAREHE 18.12.2017 MAJIRA YA SAA 08:15HRS KATIKA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE ILIYOPO  KATA YA ISAMILO WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, JOSEPH MBAGATA, MIAKA 25, MKAZI WA MTAA WA MABATINI, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUJIFANYA DAKTARI HOSPITALINI HAPO KISHA KUTAPELI FEDHA WAGONJWA ILI AWAPATIE MATIBABU, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA
AWALI ZILIPATIKANA TAARIFA KUWA SIKU CHACHE ZILIZOPITA ALIONEKANA MTU ALIYEVALIA MAVAZI YA UDAKTARI NA KUJIFANYA DAKTARI, KISHA ANAPITA WODINI KUWAONA WAGONJWA. PIA ILISEMEKANA KUWA MTU HUYO TAYARI AMECHUKUA FEDHA KIASI CHA SHILINGI ELFU THELATHINI KWA MGONJWA ILI AWEZE KUMPATIA MATIBABU.
AIDHA BAADA YA TUHUMA HIZO KUFIKA KATIKA UONGOZI WA HOSPITALI WALIWEKA MTEGO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA TAJWA HAPO JUU, AKIWA AMEVALIA MAVAZI YA UDAKTARI HUKU AKIWA AMESIMAMA NJE YA WODI YA UPASUAJI. BAADA YA DAKTARI HUYO FEKI KUKAMATWA UONGOZI WA HOSPITALI ULITOA TAARIFA POLISI, AMBAPO ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUMUWEKA MTUHUMIWA CHINI YA ULINZI KISHA KUMFANYIA UPEKUZI KWENYE BEGI ALILOBEBA NA KUKUTA MAVAZI YANAYOTUMIWA NA MADAKTARI KATIKA UPASUAJI .
POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAKE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI HUSUSANI WAGONJWA WALIOPO HOSPITALINI AKIWAMOMBA KUWA MAKINI NA WATU/ MATAPELI WA AINA KAMA HII WENYE NIA OVU DHIDI YAO. AIDHA PIA ANAWAOMBA VIONGOZI WA HOSPITAL ZOTE KUENDELEA KUTOA TAARIFA POLISI ZA WATU WANAO WATILIA SHAKA HOSPITALINI, ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.
IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Tangaza Hapa +255755300337