Header Ads


Msanii wa mchanga adai kupigwa zaidi tsh milioni 30 za urithi ya msanii mkongwe

Msanii mchanga wa muziki, Asala amefunguka kwa kueleza sababu ya kuachana na aliyekuwa meneja wake wa zamani, Tunda Man kuhu akudai kwamba meneja huyo amempotezea zaidi ya tsh milioni 30.

Muimbaji huyo amedai baada ya kukutana na Tunda Man ambaye alikuwa maneja wake alimpatia kiasi hicho cha pasa kwaajili ya muziki wake na katika makubaliano walifanikiwa kufanya kazi moja iitwayo, Subiri.
“Kusema kweli Tunda sitaki kumzungumzia tena huyo mtu katika muziki wangu kwa sababu tayari ameshanipiga sana,” alisema Asala. “Kuna pesa kama milioni 30 ambayo nilimpatia kwaajili ya muziki wangu lakini mpaka sasa sielewi chochote hata nikimpigia nyingi ni suburi, subiri, ndio maana hata project yangu mpya nimekuja mwenyewe sina meneja kabisa, bora nipambane na hali yangu,”
“Hiyo pesa mimi niliuza kitu changu za urithi, niliuza zaidi ya milioni 40 na milioni 10 tu ndio pesa ambayo niliweza kufanyia mambo yangu na nyingine niliamua kuiwekeza kwenye muziki wangu kwasababu naamini muziki ndio kitua ambacho nitakifanya kwa zangu zote,” alisema Asala.
Alisema hata tatizo na Tunda Man zaidi ya kuhitaji pesa zake ambazo anaamini zingeweza kumfikisha sehemu fulani katika muziki wake.
“Tunda bado kwangu ni kama kaka na bado hatujafikia kwenye kugombana na kushindwa kusalimiana. Mimi nachohitaji kutoka kwake ni pesa zangu tu sio mambo mengine, kama kuna sehemu aliwekeza kama anavyodai mimi nadhani hakukuwa na makubaliano ya kufanya biashara nyingine nje ya muziki, kwahiyo mimi nataka changu kwanza,” alisema Asala.
Muimbaji huyo amedai suala lake hilo bado halijafika polisi kwa sababu anaamini watafikia hatua hiyo.
Baada ya taarifa hiyo, mtandao huu ulimtafuta Tunda Man bila mafanikio kwani kila akipigiwa simu hapokei na hata alipotumiwa ujumbe mfupi ulikuwa haujibiwi. Hata hivyo bado harakati za kumtafuta zinaendelewa ili tumsikilize na yeye kwa epande wake.

No comments

Powered by Blogger.