Header Ads


Mhe. Balozi, Dkt. Ramadhani Dau awasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Mfalme wa Cambodia

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia anayewakilisha pia nchini Cambodia, Mhe. Dkt. Ramadhani Kitwana Dau (kushoto) akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mfalme wa Cambodia, Mtukufu Preah Bat Samdech Preah Boromneath NORDOM SIHAMON. Makabidhiano hayo yalifanyika tarehe 28 Novemba 2017 Jijini Phnom Pen, Cambodia.
Mhe. Balozi Dkt. Dau (wa pili kushoto) akiwa katika mazungumzo na Mtukufu Mfalme mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. Wanaoshuhudia kulia ni maafisa wa Serikali ya Cambodia na kushoto ni Afisa wa Ubalozi wa Tanzania.

Mazungumzo yao yalijikita katika kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia uliopo baina ya mataifa hayo ambao ulianzishwa rasmi mwaka 1995. Pia kuimarisha ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji. Vilevile Mtukufu Mfalme aliahidi kumpa ushirikiano Mhe. Balozi Dkt. Dau katika utekelezaji wa majukumu yake.Mhe. Balozi Dkt. Dau akimtambulisha Afisa wa Ubalozi wa Tanzania, Bw. Khatib Makenga aliyeambatana naye katika hafla ya  makabidhiano ya Hati za Utambulisho

Mhe. Balozi Dkt. Dau akipokelewa mara baada ya kuwasili jijini Phnom Penh, Cambodia. 

No comments

Powered by Blogger.