Header Ads


Kampuni ya TECNO yawaandilia wadau wake hafla ya Krisimasi.

Katika kusherehekea sikukuu za Krisimasi  na mwaka  mpya, kampuni ya simu TECNO mobile Ltd imeandaa sherehe za awali za Krisimasi maalumu  kwa  wadau wake.

TECNO iliwakutanisha wadau na mashabiki wake kutoka katika mitandao ya kijamii mbalimbali ikiwemo, Twitter, Instagram, Facebook na TECNO spot katika hafla fupi iliyopewa jina la “TECNO Fans Night” iliyofanyika katika uwanja wa burudani wa ESCAPE ONE Mikocheni.
 Kusudio likiwa ni kuwapongeza na kutoa shukurani kwa wadau na mashabiki kwa kuwa pamoja na kampuni hiyo kwa mwaka mzima na kuwa mabalozi wa kampuni hiyo ya simu.
 Sherehe hiyo ilikua na ugeni wa mtangazaji maarufu afahamikae kwa jina la “Lil Ommy” Omary Tambwe wa Times FM akiwa kama shereheshaji wa sherehe hiyo iliyoandaliwa na TECNO. Hafla hiyo  ilipambwa kwa  michezo, burudani na chakula cha jioni  huku zawadi  mbalimbali zikitolewa  kwaaajili ya mshabiki na wadau wa kampunI hiyo ya TECNO waliofika.
“Kiukweli nimefurahi kuwa hapa, kuungana na wenzangu. Nimepata nafasi ya kuongeza marafiki usiku wa leo, asante sana TECNO” – alisema mmoja wa wadau/shabiki wa TECNO.

“Mpaka sasa kwa mwaka huu tumeweza kuwa na ushawishi sana kwa upande wa mitandao ya kijamii na tumeweza kuwapa kile wadau na mashabiki wetu wanapenda, nahisi ndicho kilichoweza kutupa mabalozi kama hawa. Kiukweli hatuwezi kuwa sisi bila ya watu kama hawa ambao waipenda bidhaa na kampuni hivi, hivyo ni sawa tu kama na sisi kama kampuni tukatenga muda ili kuweza kuungana nao kusherehekea mafanikio na pia sikukuu” – Meneja mahusiano.
TUNAWATAKIA KHERI YA KRISIMASI
Tazama video ya yaliojiri 

 Xmas party

No comments

Powered by Blogger.