Header Ads


Kampuni mbalimbali Mkoani Tabora zimetakiwa kushiriki katika zoezi la upandaji miti

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri.
............
NA TIGANYA VINCENT RS TABORA

SERIKALI Mkoani Tabora imezitaka Kampuni zote zinazoendesha shughuli zake katika eneo hilo kuhakikisha zinashiriki katika zoezi la upandaji miti kama sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii ambayo ni wadau na watumiaji wa huduma zao badala ya kujali maslahi yao pekee.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akiongoza watumishi wa Ofisi yake, Manispaa ya Tabora na wananchi katika zoezi la upandaji miti maji 500 iliyotolewa na Kampuni ya Usambazaji wa Gesi ya Manji,s kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali.

Alisema kuwa kitendo cha Kampuni ya Usambazaji wa Gesi ya Manji’s ya kutoa miti 500 na kushirikiana na watumishi katika upandaji kwenye barabara kutoka Tabora kwenda Urambo kinatakiwa kiigwe na wafanyabiashara na Kamapuni zote zinazotoa huduma mkoani humo.

Mwanri alisema kuwa athari katika mazingira haitaishia katika kuwaathiri wananchi pekee pia itasababisha biashara na shughuli katika Kampuni zao kuathirika na hivyo suala la upandaji na utunzaji wa miti linapaswa kuwa sehemu ya mipango yao.

Alisema kuwa upandaji wa miti uwe na tija hauwezi kuwa wa kundi fulani pekee bali unapaswa kuwa jamii yote wakiwemo wanaotoa huduma mbalimbali na wale wanaoendesha biashara katika Mkoa wa Tabora.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora alisema kuwa mapema wiki ijayo kutakuwepo makundi mbalimbali katika maeneo tofauti mkoani humo yatakayohakikisha yanapanda miti yote iliyopo kwenye vitalu kabla ya msimu wa mvua haujamalizika.

Alisema kuwa kundi la kwanza litawashirikisha wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo  ambao watashiriki kupanda miti ya matunda katika Shule zao zote na vyuo na miti mingine ikiwa ni sehemu ya kutoa pia elimu kwao juu ya kujali mazingira.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa kundi lingine litakuwa ni kwa watumishi , Vyama vya Msingi na Kampuni za Ununuzi wa Mazao kupanda miti na kwa kila mwananchi kupanda na kuonyesha miti aliyopanda katika eneo lake.

Kwa upande wa Msambazaji Mkuu Kutoka Kampuni ya  Gesi ya Manji’s Johnson Mtei alisema kuwa katika wanendelea kuunga juhudi za Serikali ,kila mwaka watakikisha wanatoa miche ya miti 500 kwa ajili ya upandaji maeneo mbalimbali mkoani Tabora ili kuufanya Mkoa huo uwe wa kijani.

Alisema kuwa wao wanatambua kuwa ukataji hivyo wa miti  unatishia kuigeuza Tabora kuwa sehemu ya Jangwa na ndio maana wameamua kuuunga mkono juhudi za Serikali ikiwemo ya Mkoa katika manapanda miti ili kuridisha uoto wa asili.

Mtei aliongeza kuwa Kampuni imeamua kuendesha Kampeni ya uapndaji miti na  Matumizi ya Gesi katika maeneo ya vijijini ili kunusuru mistu asili na kurudishia katika maeneo ambayo imekatwa.

Aliongueza kuwa sanjari na hilo wamepunguza bei ya gesi yao kwa ajili ya kuwawezesha wananchi wengi waone kuwa kila mtanzania anaweza kupika kwa kutumia gesi na sio matajiri pekee.

Aidha alitoa wito kwa Serikali kuzisaidia taasisi mbalimbali kama Shule, Vyuo na Magereza kuanza matumizi ya gesi kwa ajili ya kuokoa mistu ambayo imekuwa ikikatwa kwa ajili ya kupata kuni.

Mtei aliwashauri viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na maeneo mengine kuhakikisha kabla ya watu wa mipango miji hawajapitisha ramani za ujenzi wahusika wapande miti kwanza ndio waendelee na hatua nyingine ili kujenga tabia ya watu kupenda kupanda miti na kulinda mazingira.

Alisema kuwa ni vema wakajenga tabia ya wanapokaa sehemu wanaacha kumbkukumbu ambayo hata wakiwa hawapo wanakumbuka siku zote.

No comments

Powered by Blogger.