JKCI yafanya upasuaji wa moyo uliokaa upande - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Friday, 1 December 2017

JKCI yafanya upasuaji wa moyo uliokaa upande

 Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)na wenzao wa  Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia wakifanya upasuaji kwa mtoto ambaye vyumba vyake vya  moyo havijakamilika na hivyo damu kwenda kwa wingi kwenye mapafu katika kambi ya siku tano ya matibabu ya moyo iliyomalizika leo katika Taasisi hiyo. 
 Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na mishipa ya damu  kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia wakimfanyia mgonjwa  upasuaji  wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) katika kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo iliyomalizika leo katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa  16 wamefanyiwa upasuaji  na hali zao zinaendelea vizuri kati ya hao watoto ni tisa  na watu wazima saba.
Mwanzilishi wa Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia Russel Lee akiongea na waandishi wa Habari kuhusu upasuaji wa moyo wa mtoto ambao umekaa upande wa kulia na mishipa yake ya damu chafu na safi imeingiliana katika upasuaji huo wameweza  kulinda mapafu yalikuwa yanapokea  damu kwa wingi kutoka kwenye mishipa ya moyo na mtoto kawekewa kifaa ambacho kitamsaidia moyo wake kufanya kazi vizuri (Pace Maker). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto Godwin Sharau. 


Picha na JKCI 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages