Header Ads


Dk. Charles Kimei asema hataongeza mkataba wake mara utakapofikia ukomo Mei 31, 2019.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (kulia) akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam akizingumzia mchakato wa kutafuta Mkurugenzi Mpya wa Benki hiyo atakapostaafu Mei 31, 2019, kushoto ni Mkurugenzi wa Mikopo James Mabula.

Na Abraham Ntambara, Dar es Salaam

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei ametangaza kuwa hataongeza mkataba wake mara utakapofikia ukomo Mei 31, 2019.

Amesema hayo Desemba 28,2017 jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema amekuwa katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka 20 hivyo umekaribia wakati wake wa kumwachia mtu mwingine.

“Nimekuwa mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB kwa takribani miaka 20 sasa, hivyo wakati umekaribia kwangu mimi kumwachia mtu mwingine nafasi hii na mimi kuendelea kufanya majukumu mengine,” amesema Dk. Kimei.
Amesema Kufuatia sera ya kurithisha nafasi ya mkurugenzi mtendaji wa Benki yetu hii, ifikapo Januari 2018, Bodi ya Benki inalazimika kuanza mchakato kwa ajili ya kujaza nafasi hii muhimu kwa mustakabali wa Benki ya CRDB,”

Dk. Kimei amesema mchakato wa kumtafuta Mkurugenzi Mtengaji mpya umekwisha aanza na sababu ya kuanza mapema ni ili kuhakikisha zoezi linafanyika kwa uangalifu na kutoa muda wa kutosha wa kupata uidhinisho wa mamlaka husika kwa mtu atakayechaguliwa kushika nafasi hiyo.

Amewahakikishia wateja wa benki hiyo na watanzania kwamba benki ni salama na itaendelea kuwa salama.

“Tunatangaza hili mapema ili kuepusha dhana au hisia ya kwamba mkurugenzi mkuu anaondoka kwa vile kuna tatizo, au benki inaweza kuyumba. Niko kwa takribani miezi 18 na mioyo ya wateja ibaki na amani,” amesema.
Baadhi ya wakurugenzi na wafanyakazi wa benki hiyo wakifuatilia mazungumzo ya mkurugenzi mtendaji wa CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.