Chauru yadhamiria kuinua kilimo cha mpunga msimu ujao - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka

Habari za Hivi Punde

Tangaza Hapa +255755300337

Post Top Ad

Post Top Ad


Thursday, 28 December 2017

Chauru yadhamiria kuinua kilimo cha mpunga msimu ujao

 Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha umwagiliaji Ruvu (CHAURU)Mkoani Pwani,Sadala Chacha akionekana pichani kuzungumza na wanachama wa chama hicho (hawapo pichani),wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Baadhi ya wanachama wa chama cha ushirika cha umwagiliaji Ruvu (CHAURU)Mkoani Pwani wakiwa kwenye mkutano mkuu wa chama hicho.
(Picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

CHAMA cha ushirika cha umwagiliaji Ruvu (CHAURU )mkoani Pwani,kimedhamiria kuinua kilimo cha mpunga na kuingia kwenye soko la mchele badala ya mpunga ili kumnufaisha mkulima wa zao hilo katika msimu ujao .

Aidha chama hicho kimenunua trekta lililogharimu sh.mil.77 ,kwa ajili ya kuwasaidia wanachama wa ushirika huo kwa ajili ya kulima kirahisi na kuondokana na gharama za kukodi matrekta .

Akizungumza katika mkutano mkuu wa chama ,;mwenyekiti wa CHAURU ,Sadala Chacha alisema msimu uliopita wa mwaka 2016/2017 walipata changamoto kwa baadhi ya mifereji kukumbwa na mafuriko hali iliyosababisha wakulima wanaolima kwenye mifereji hiyo kushindwa kuvuna.

Alisema kutokana na mvua nyingi na mafuriko jumla ya hekari 1,700 ziliathirika.

Chacha alieleza ,kwa wakulima waliovuna nao walipata changamoto ya mpunga kuingiliana kwa wakati mmoja na kukosa maeneo ya kuanika .

";Kutokana na changamoto hizi tunajipanga katika msimu unaokuja kununua maturubai ya kutosha na kuweza kuanika kwa wakati na kuziba mifereji iliyokuwa ikiingiza maji ".

Chacha alisema mkakati mwingine waliojiwekea  ni kutoka kwenye kuuza mpunga na kuuza mchele ili kupata soko na kujiongezea mapato.

Alieleza hatua hiyo inafuatia baada ya kugundua kuwa kuuza mpunga badala ya mchele kumesababisha wakulima kupunjika na kutofaidika na kazi kubwa wanayofanya.

Chacha alisema ,hawawezi kufanikiwa kama hawataboresha kilimo hicho na kuwa cha kisasa na kutumia zana bora ndipo walipoamua kutengeneza kinu na kununua trekta litakalowawezesha kufikia malengo yao.

Akizungumzia kuhusiana na mapato na matumizi kwa mwaka 2016 alisema walipata mapato ya zaidi ya milioni.309.234 na matumizi yalikuwa ni milioni .2 .857.

"Tangu kuanzia mwezi februari 2016 tulikuwa na hisa milioni 5.3 ambapo kwasasa tuna hisa ya milioni.20 na faida ni zaidi ya milioni. 33" alifafanua Chacha.

Nae mkaguzi msaidizi daraja la pili Samwel Mgeni ,kutoka shirika la ukaguzi na usimamizi wa vyama vya ushirika (COASCO),alisema CHAURU imepiga hatua kwani ni moja ya ushirika unaofanya ukaguzi wa mahesabu yake. 

Aliwashauri  kuangalia vyanzo vya mapato,kuwa na elimu ya masuala ya fedha na wapunguze matumizi yasiyo ya lazima.

"Vyama vingi vya ushirika havifanyi ukaguzi lakini CHAURU ni moja ya ushirika unaojitambua na kusimamia masuala ya ukaguzi ,kuwa na vyanzo vya mapato na hakika watafika mbali" alisema Samwel.

Baadhi ya wanachama wa CHAURU akiwemo William Mserikali na Rogati Chuwa ,waliwataka maafisa ugani kutoka maofisini na kwenda kuwatembelea wakulima hao ili kujua changamoto wanazokabiliana nazo.

Afisa tarafa ya Chalinze ,Thomas Mollel alisema ushirikiano na umoja ndio nguzo kwa ushirika huo .

Mollel alisema, ili ushirika ulete manufaa baadhi yao waachane na tabia ya kuwarudisha nyuma viongozi waliopo madarakani.

Chama cha ushirika wa wakulima wa umwagiliaji (CHAURU)kilichopo Ruvu,kinajishughulisha na kilimo cha umwagiliaji maji wa zao la mpunga katika mashamba na hadi sasa kina wanachama 894.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Tangaza Hapa +255755300337