Benki ya TPB yachezesha droo ya pili ya Western Union - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka

Habari za Hivi Punde

Tangaza Hapa +255755300337

Post Top Ad

Post Top Ad


Thursday, 21 December 2017

Benki ya TPB yachezesha droo ya pili ya Western Union

Benki ya TPB  Desemba 21, 2017 imechezesha droo ya pili ya Western Union na kupata washindi 7 kutoka matawi mbalimbali .

Washindi 5 walipata simu za mkononi na 2 walipata kompyuta mpakato.

Majina hayo yalitajwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa benk hiyo Bw. Mshamma Mshamma na kusimamiwa na Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed.

Washindi waliojishindia simu za mkononi aina ya Samsung J5 ni Bi. Elizabeth Lugendo kutoka Dar es Salaam, Bw.Frank Tetea kutoka Korogwe Tanga, Bw, Jafari Msaki kutoka Arusha, Bi. Rose Maluka kutoka Dodoma na B. Anna Kasoga kutoka Ifakara -Morogoro.

Washindi wawili waliojishindia kompyuta mpakato ni Bw. Justine Muyanza kutoka Mwanza na Bw. Abdul Hurey kutoka Arusha.
 Ofisa Mauzo wa Benki ya TPB Bw. Nelson Mwakilasa akimwaga kuponi za droo ya pili Western Union wakati wa kumtafuta mshindi wa droo hiyo ilifanyika Desemba 21,2017 katika ofisi za Benk hiyo Jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa huduma ya Western Union kutoka Benki ya TPB. Editha Lunyungu (kushoto) akihakiki majina ya washindi kwenye kopyuta  mpakato wakati wa kumtafuta mshindi wa droo ya pili Western Union wakati wa kumtafuta mshindi wa droo hiyo ilifanyika Dar es Salaam.
  Kaimu ofisa Mtendaji Mkuu kutoka Benki ya TPB, Bw. Mshamma  Mshamma (kushoto) akisoma jina la mshindi katika droo ya pili ya Western union. kulia anae shuhudia ni  mwakilishi kutoka Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed
   Kaimu ofisa Mtendaji Mkuu kutoka Benki ya TPB, Bw. Mshamma  Mshamma (kushoto) akisoma jina la mshindi katika droo hiyo.
 Ofisa Mauzo wa Benki ya TPB Bw. Nelson Mwakilasa akichanganya kuponi za droo ya pili Western Union wakati wa kumtafuta mshindi wa droo hiyo ilifanyika Dar es Salaam.
 Kaimu ofisa Mtendaji Mkuu kutoka Benki ya TPB, Bw. Mshamma  Mshamma (kushot) akitaja majina ya washindi katika droo ya pili ya Western union.
Pcha ya pamoja.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Tangaza Hapa +255755300337