Wakulima wa mpunga wapewa siku sita kukamilisha mifereji ya maji mashambani mwao. - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Monday, 13 November 2017

Wakulima wa mpunga wapewa siku sita kukamilisha mifereji ya maji mashambani mwao.

Picha na Maktaba.
...
NA TIGANYA VINCENT RS –TABORA
WAKULIMA wa Mpunga katika Mradi wa Umwagiliaji wa Ussoke Mlimani na Yelayela ambao hadi hivi sasa hawajakamilisha uchimbaji wa mifereji inasambaza maji kutoka mfereji mkuu kwenda kwenye mashamba yao wametakiwa kuhakikisha wamekamilisha zoezi ndani ya wiki hii.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni katika eneo la mradi lilipo Ussoke Mlimani na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo  Margaret Nakainga  wakati wa kikao kati ya Uongozi wake na Wakulima wanachama mradi huo wa umwagiliaji.
Alisema kuwa baada ya muda waliokubaliana katika kikao hicho kumalizika , watakaokuwa wameshindwa wata hatua na viongozi wao kulingana na maamuzi waliofika ili wasiendelee kuwa kikwazo cha kutaka kurudisha nyuma ufanisi wa mradi huo uliotumia fedha nyingi.
Nakainga alisisitiza kuwa uchuleweshaji wowote unaweza kusababisha baadhi ya wakulima washindwe kulima kwa sababu ya mkulima aliyemtangulia hajachimba mfereji ambao utaruhusu maji yapite kwake kisha yaende kwa jirani yake.
“Natarajia kuja kukagua siku ya Ijumaa kama mtakuwa mmekamilisha kuchimba mifereji kama tulivyokubaliana katika kikao hiki….atakayekuwa hajakamilisha tutaona ni hatua gani tuchukue ili asije akawa kikwao kwa wanamradi wengine” alisisitiza DED.

Naye Mwenyekiti wa Mradi huo Bryson Kazala aliwataka wakulima ambao hawajakamilisha maandalizi ya mashamba yao kufanya hivyo mapema la sivyo watalazimika kuwanyang’ana na kuwagaiwa waliotayari kuyaendeleza.

Alisema kuwa ni lengo la mradi huo ni kutaka kila eneo lililopimwa lifanyekazi ya uzalishaji ili hatimaye waweze kuishawishi Serikali ipanue eneo la mradi kwa ajili ya kuingiza wanachama wengi zaidi.

Kazala alisema kuwa ni vema kila mkulima aliyeomba shamba na kupatiwa akahikikisha ndani ya muda walijipangia anaweka eneo lake vizuri tayari kwa ajili ya kilimo hicho.

Kwa upande wa Katibu wa Mradi huo Rajab Karunguyeye alisema kuwa ikiwa wanachama waliojiandikisha katika mradi huo watawajibika ipasavyo wataondoa suala la kuagiza mchele kutoka nje ya kijiji na kuwa ziada ya kuwauzia watu wengine.

Mradi huo ambao umegharimu zaidi ya shilingi milioni 800 una mashamba ambayo yana ukubwa wa hekta 211 ambayo ni kwa ajili ya kilimo cha kisasa cha umwagiliaji mpunga.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo  Nakainga ametoa wito kwa Wakulima wote wilayani humo kutumia mvua zilizoanza kunyesha kulima mazao mazao mchanganyikoa kwa ajili ya chakula na biashara.

Alitaja baadhi ya mazao hayo kuwa ni mihogo, viazi vitamu, mahindi , alizeti , pamba, karanga na tumbaku kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanakuwa na mazao ya aina mbalimbali ambayo yatakuwa chanzo cha chakula na wanaweza kuyauza kwa ajili ya uboreshaji wa maisha ya familia zao.

Nakainga aliwataka wanapolima wazingatie maoni ya wataalamu ili waweze kupata mazao bora na mengi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages