Wahamiaji haramu wanaswa wakihaha kutafuta chakula - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Thursday, 9 November 2017

Wahamiaji haramu wanaswa wakihaha kutafuta chakula

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

RAIA 18 kutoka nchini Ethiopia wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Pwani ,kwa kosa la kuingia nchini bila kibali .

Kamanda wa polisi mkoani Pwani Jonathan Shanna alisema wahamiaji hao walikamatwa eneo la Pera kata ya Pera wilaya ya kipolisi chalinze wakiwa wamejitokeza kwenye barabara kuu wakitafuta chakula.

Alisema baada ya kukaa porini muda mrefu bila ya kula wakimsubiri mwenyeji wao ndipo walikuwa wakitaabika kwa njaa.


Shanna alielezea katika tukio jingine ,jeshi la polisi mkoani hapo ,linawashikilia watu wawili kwa kukutwa na mali ya wizi katika nyumba wanazoishi.

Shanna aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Philbert Lyimo na Doris Urasa, na kuwa wengine wanne walikimbia .

"Wawili hawakupatikana majina yao na wengine wawili ni bwana na bibi Novatus Lyimo ambao wanatuhumiwa kwa wizi na uvunjaji katika maeneo mbalimbali katika wilaya ya kipolisi chalinze" alisema.

Polisi wamebaini mtandao wa  watu unaojihusisha na uvinjaji wa bar na grocery na matukio ya unyang'anyi wa kutumia nguvu nyakati za usiku, ambapo katika msako huo kukamata gari la wizi lililotelekezwa lenye namba T. 355 DEB aina ya Toyota Primio.

Shanna alisema gari  hilo inasadikiwa lilitelekezwa na watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliokuwemo kwenye gari hiyo na kukimbilila porini baada ya kugundua wanafuatiliwa na polisi ambao walikuwa wamewatilia shaka.

Alisema baada ya polisi kuchukuwa gari hilo walibaini kuwa namba zilizokuwa zimewekwa zilikuwa za kugushi na namba namba halali ilikuwa ni T. 447 BTM, mali ya Novatus Lyimo mkazi wa kimara makazi mapya.


Alieleza mali zingine za wizi zilizokutwa zimeibwa maeneo mbalimbali ni Pikipiki  namba  MC 623 BKC, mota ya kuvutia maji, radio aina ya son, grand chupa tatu kubwa, deki aina ya MPG4, chupa za wine 10, brenda moja na drill mashine, ambavyo vyote vimetambuliwa waliovinjiwa katika maeneo yao.

Kamanda alitaja vitu vingine vilivyokamatwa na bado havijatambuliwa na wahusika kuwa ni spika kubwa aina ya sony na radio moja ya gari.

Pia Tv flat mbili, jenereta mbili, projecta moja, king'amuzi kimoja, EFD mashine moja, maiki mbili, friji moja, viti vya serengeti nane, buti za polisi, filimbi ya polisi na koti la polisi linalotumiwa wakati wa mvua .


Aliendelea kutaja vitu hivyo ambavyo bado havijatambuliwa na wahusika kuwa ni bia kreti saba, mkasi mkubwa wa kukatia makufuli, mtalimbo mmoja na pombe kali  na waini aina mbalimbali.

Shana alitoa onyo kwa watu wanaojihusisha na matukio ya uhalifu ikiwemo usafirishaji wa binadamu ndani ya mkoa wa Pwani kuacha mara moja na kutafuta kazi nyingine ya kufanya. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages