Ukatili dhidi ya wanawake tatizo kubwa hapa nchini-Ndugulile - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Tuesday, 21 November 2017

Ukatili dhidi ya wanawake tatizo kubwa hapa nchini-Ndugulile

 Naibu Waziri wa Afya, Maendelego ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akitoa hotuba ya ufunguzi wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Dawati la Jinsia na Watoto linalosimamiwa na Jeshi la Polisi Tanzania.
 Mkurugenzi wa CDF Koshuma Mtengeti akikabidhiwa cheti cha mdau wa Dawati la Jinsia aliyetukuka na Mhe. Naibu ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dr. Faustine Ndugulile.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendelego ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Maendeleo mara baada ya kupokea vyeti kutoka Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Dawati la Jinsia na Watoto linalosimamiwa na Jeshi la hilo. 
 Naibu Waziri wa Afya, Maendelego ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na Makamishina wa Jeshi la Polisi wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Dawati la Jinsia na Watoto linalosimamiwa na Jeshi la hilo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendelego ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akipokea Maandamano ya Jeshi la Polisi wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Dawati la Jinsia na Watoto linalosimamiwa na Jeshi la hilo.

Na Anthony Ishengoma
Takwimu za shirika la Afya Duniani zinaoenesha kuwa asilimia 35 ya wanawake ulimwenguni ni wahanga wa vipigo na  ukatili wa kingono au vyote kwa pamoja wakati hapa nchini Tanzania taarifa ya hali ya watu na Afya ya waka 2015 inaonesha kuwa asilimia 40 ya wanawake wenye umri kati ya miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kupigwa katika kipindi cha mwaka mmoja.
Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulile amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano Mkuu wa  wa mwaka wa Dawati la Jinsia na Watoto wa Jeshi la Polisi unaondealea kwa siku tatu.
Aidha Mhe. Ndugulile ameongeza kuwa pamoja na kuwepo ukatili wa kingono na vipigo kwa wanawake lakini pia vitendo vya ukeketaji bado ni tatizo kubwa hapa nchini akisema  liko juu kwa kiwango cha asailimia 30 akiutaja mkoa wa Manyara kuwa na  kiwango cha ukeketaji kwa asilimia 58.
Aidha Mikoa mingine inayaoongoza kwa vitendo vya ukeketaji ni pamoja na Mkoa wa Dodoma kwa sailimia 47,Arusha asilimia 41 ikifutiwa na Mkoa wa Mara na Singida yenye kiwango cha asilimia 32.  
Aidha ameonya kuwa ukatili wa kijinsia haukubaliki akitaja kuwa bado kuna kiwango kikubwa cha ukatili hapa Nchini na kinagharimu Jamii na Taifa letu katika Nyanja za kijamii, kisiasa na kiuchumi ikiwemo kuzorota kwa afya ya walengwa.
Wakati huhuo Mwakilishi wa Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Kamishina wa Polisi Jamii hapa Nchini Mussa Ally Musa amesema kuwepo na ongezeko kubwa la taarifa za ukatili wa kijinsia na unyanyasaji kwa  watoto tangu kuanzishwa kwa dawati hilo hapa Nchini ambapo kwa kipindi cha Januari-Desemba 2016 jeshi la polisi limepokea matukio 10,551 ya ukatili wa kijinsia kwa watoto ukilinganisha na matukio 9541 katika kipindi kama hicho 2015 na 2488 ya mwaka 2014.
Aidha ameitaja mikoa inayoongoza kwa matukio haya kuwa ni mkoa wa Moarogoro 1403, Rukwa 850, Singida 697,Iringa 649 na Dodoma kiwango cha matukio hayo ni 609 akiongeza kuwa kwa upande wa Tanzania visiwani Mikoa inayoongoza ni Mkoa wa Kusini pemba, Kusini unguja na Kasikazini unguja.
Aidha kamishina Musa ameyataja makosa ya ubakaji kuwa ndiyo yanayoongoza ambapo Jeshi la Polisi mpaka sasa limepokea jumla ya matukio 4,423 ya ubakaji , shambulio 1,801 na shambulio la kudhuru mwili 1,021 na matukio yan kujerui 819.    
Pamoja na ongezo hilo la matukio hayo pia dawati la jinsia la jeshi la polisi limekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ushirikiano mdogo kutoka kwa familia husika, uchache wa vifaa na majengo, uelewa mdogo wa wananchi na watendaji wa serikali pamija na ukosefu wa meaneo ya kuifadhi waanga wa ukatili.

Aidha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Faustine Ndugulile ameongeza kuwa changamoto inayokabili Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi ni ufinyu wa bajeti, upungufu wa rasilimali watu, akisema serikali itaendelea kufanyia kazi mapungufu yaliyoplo huku akitaja juhudi mojawapo ni uwepo wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages