Timu nane zafuzu robo fainali Spanest Cup - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Thursday, 9 November 2017

Timu nane zafuzu robo fainali Spanest Cup

 Mratibu wa mashindano kutoka Spanest, Godwell Ole Meing’ataki akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi wa timu zilizoingia hatua ya robo fainali ya kombe la Spanest.
 Mratibu wa mashindano kutoka Spanest, Godwell Ole Meing’ataki akikabidhi moja ya seti ya jezi kwa nahodha wa timu ya soka ya kijiji cha Ilolo Mpya, Esau Mwashambwa.
Mratibu wa mashindano kutoka Spanest, Godwell Ole Meing’ataki akionyesha kombe ambalo linyakuliwa na bingwa wa mashindano ya kombe la kupiga vita ujangili la Spanest ofisi kwake.

NA DENIS MLOWE, IRINGA
 
JUMLA ya timu 8 zimefuzu hatua ya robo fainali ya mashindano ya kombe la kupiga vita ujangili ya Spanest Cup 2017 kutoka katika tarafa za Idodi na Pawaga yanayoandaliwa na mradi wa kuboresha mtandao wa hifadhi zilizo kusini mwa Tanzania (SPANEST) kwa kushirikiana na Hifadhi ya Taifa Ruaha.
 
Akizungumza wakati wa kutaja timu za vijiji zilizofanikiwa kuingia hatua ya robo fainali na kuwazipatia vifaa vya michezo, Mratibu wa mashindano hayo kutoka Spanest, Godwell Ole Meing’ataki  alisema kuwa baada ya hatua za kwanza na pili kumalizika kuna timu za vijiji ambazo zilileta rufaa katika kamati kulalamikia mechi zaidi ya sita zilizovunjika.
 
Meing’ataki alisema kuwa mechi zilizovunjika zilitokana na vurugu za mashabiki, usalama wa waamuzi hivyo kamati ilikaa na kuamua ni timu gani ambazo zinastahili kuendelea na mashindano kwa kuzipatia pointi timu ambazo zilistahili kutokana na timu husika kuwa chanzo cha vurugu.
 
Alisema kuwa kuvunjika kwa baadhi ya michezo hiyo ni kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mashabiki wa wa baadhi ya vijiji kuwa chanzo cha vurugu kutokana na kutokuwa wavumilivu pindi maamuzi yanapokuwa tofauti.
 
Aidha alisema kuwa chanzo kingine ni changamoto ya waamuzi kuonyesha upendeleo kwa baadhi ya timu na kutoa maamuzi ambayo wakti mwingine husababisha kuamsha hisia kali na kuleta vurugu na baadaye kuvunjika kwa mchezo husika.
 
“Natoa wito kwa wachezaji na viongozi na mashabiki wabadilikena kuzingatia kanuni kwani hatua tuliyofikia tutakuwa wakali zaidi katika kusimamia kanuni na tunaahidi kuyafanyia kazi baadhi ya malalamiko yaliyondani ya uwezo wetu yakiwemo ya waamuzi.” alisema
 
Meng’ataki alizitaja timu ambazo zimeingia katika robo fainali ya mashindani hayo kutoka Tarafa ya Idodi kuwa ni timu za kijiji cha Mapogolo, Malinzanga, Mahuninga, na Idodi waliongea kama washindi bora kwa walioshindwa (Best Loser)
 
Alizitaja timu ambazo zimeingia robo fainali ya mashindano hayo kutoka tarafa ya Pawaga kuwa ni Ilolo Mpya, Itunundu, Kinyika na Mboliboli ambao wanapewa nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa kutokana na kiwango chao walichokionyesha tangu kuanza kwa mashindano hayo.
 
Aliongeza kuwa kamati imetoa vifaa vingine kwa timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ambayo itaanza rasmi siku ya jumamosi kwa kupatiwa jezi seti moja kwa kila timu iliyoingia robo fainali.
 
Meing’ataki alisema kuwa Mashindano hayo ya mpira wa miguu yameandaliwa kwa lengo la kuimarisha uhifadhi kwa wananchi kupitia mpira wa miguu kutokana na mwitikio mkubwa hasa katika kutimiza lengo la kuwapatia elimu ya ujangiri wananchi kuokoa tembo waliopo katika hifadhi za ruaha.
 
Katika mashindano hayo yanayotarajia kufika kilele chake Novemba 19 mwaka huu mshindi wa kwanza anatarajia kuondoka na kitita cha shilingi milioni 1, jezi seti moja,mipira miwili, cheti, medali za dhahabu na safari ya kutembelea hifadhi ya taifa ya Ruaha.
 
Mshindi wa pili ataondoka na mpira mmoja, cheti, medali ya shaba na fedha tasllimu shilingi laki 7 huku mshindi wa tatu akiondoka na mpira mmoja, cheti, medali na fedha taslimu shilingi laki 5 na mshindi wa nne ataondoka na mpira mmoja, cheti cha ushiriki na fedha taslimu shilingi laki 3.
 
Aidha kutakuwa na zawadi kwa ajili ya mfungaji bora atapata mpira mmoja na fedha laki 1. Muamuzi bora atapata seti ya jezi ya uamuzi na shilingi laki 1 na zawadi kwa ajili mchezaji bora laki 1.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages