TECNO kushirikiana na Vodacom kuitambulisha Phantom 8 Nchini - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Saturday, 11 November 2017

TECNO kushirikiana na Vodacom kuitambulisha Phantom 8 Nchini

Kampuni  kinara ya simu za mkononi  TECNO  imeungana na Vodacom kutambulisha toleo jipya TECNO Phantom 8, Simu hiyo iliyozinduliwa nchini Dubai imetambulishwa rasmi nchini Tanzania katika duka la TECNO SMART HUB lililopo Mlimani City mapema mwezi huu.

Akizungumza wakati wa utambulisho ,  Afisa mahusiano wa TECNO , Eric Mkomoya  amesema ‘’ TECNO tumeitambulisha rasmi Phantom 8 nchini Tanzania leo tukiwa na mshirika wetu wa matoleo ya Phantom nchini , Vodacom .Tumetengeneza  simu bora yenye hadhi, tunayofuraha kuwataarifu wateja wetu kuwa  Phantom 8  inapatikana katika Smart Hubs za TECNO na maduka yote ya Vodacom nchini.’’ Alihitimisha
 Afisa mahusiano wa TECNO , Eric Mkomoya.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu kitengo cha mahusiano Vodacom Jackline amesema ‘’ TECNO inataraji wateja wake kufurahia matumizi ya toleo jipya la simu janja iliyopo sokoni ambayo tayari imejipatia umaarufu kwa kupokelewa vizuri  sehemu mbali mbali nchini Tanzania  .Vodacom inawazawadia  meseji  300 , 5GB  za kuperuzi mtandaoni ,  na dakika 300 za kupiga mitandao yote kwa  wateja watakao nunua Phantom 8 katika maduka ya Vodacom yaliyopo nchini kote .
 Mkuu kitengo cha mahusiano Vodacom Jackline (katikati)
Phantom 8  ina  6GB RAM,Betri yake  ina uimara wa 3500 mAh za kuhifadhi chaji kwa  muda mrefu, 64 GB ROM, inayoipa simu uwezo wa  ziada wa kuhifadhi data  kufikia 2TB , Inavuta picha iliyombali kwa ukaribu bila kupoteza muonekano  halisi mara 10 zaidi ya simu za kawaida . Phantom 8 ina muundo na mtindo wa kuvutia hasa rangi yake yenye mng’ao wa almasi
 Afisa mahusiano Eric Mkomoya na Mkuu kitengo cha mahusiano Vodacom Jackline
Ushirikiano baina ya TECNO na Vodacom umekua wa kudumu ambapo awali waliitambulisha Phantom 6 na 6+ sasa wanakuletea Phantom 8 inayotikisa soko ikiwa na 20MP kamera ya mbele na  12MP +13 MP  kamera zake 2 za nyuma.
Mwandishi wa habari Asia Matona alijinyakulia zawadi ya Phantom 8 kwa hisani ya TECNO na Vodacom.
Mwandishi wa habari Asia Matona akifurahia zawazi yake ya simu TECNO Phantom 8 aliyoshinda. 


Kwa maelezo zaidi kuhusiana na TECNO tafadhali tembelea tovuti yetu ya http//www.tecno-mobile.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages