Serikali yazindua ndege maalumu itakayofanya doria eneo la bahari kuu kudhibiti uvuvi haramu - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Friday, 10 November 2017

Serikali yazindua ndege maalumu itakayofanya doria eneo la bahari kuu kudhibiti uvuvi haramu

Serikali imezindua mkakati unaolenga kutokomeza uvuvi haramu kwa kuanzisha operesheni ya kutumia ndege maalumu itakayofanya doria katika eneo la bahari kuu.

Akizungumza wakati wa kuzindua safari ya ndege ya kutoka nchini Mauritius iliyotua hapa nchini, kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kufanya doria ya majini, Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega alisema lengo ni kudhibiti uvuvi haramu katika eneo la bahari kuu.

Alisema Serikali ya awamu ya tano imejipambanua juu ya ulinzi wa rasilimali za nchi, ikiwamo meli ya uhakika ya majini, licha ya kukumbwa na dhoruba kubwa.

Amesema kutokana na hali hiyo ndiyo maana wameunganisha nguvu kwa pamoja kati yao na Ukanda wa nchi za Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi kudhibiti uvuvi haramu kwa njia zote.“Tunaruhusu ndege ya doria leo, ili kuongezea nguvu njia za kudhibiti wavuvi haramu, tulianza kwa njia ya bahari na sasa ni kwa njia ya anga.

“Changamoto ya uvuvi haramu ni kubwa, mtu anapiga bomu kwenye matumbawe anafanya uharibifu ambao kuyatengeneza tena yanachukua zaidi ya miaka 100, huku yeye akiharibu kwa dakika tano, ” alisema Ulega.

Ulega alisema uharibifu huo ndiyo unachangia kuwatia umasikini wavuvi wengi kwa sababu siyo rahisi kupata samaki karibuni na kulazimika kwenda mbali ambako siyo rahisi kufika bila kuwa na vyombo maalumu.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akishuka kwenye ndege maalumu itakayofanya doria katika eneo la bahari kuu kudhibiti uvuvi haramu mara baada ya kuikagua ndani.
 Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed na Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega pamoja na viongozi mbalimbali wakiangalia ndege maalumu ya doria katika eneo la bahari kuu kudhibiti uvuvi haramu.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya operesheni ya kutumia ndege maalumu itakayofanya doria katika eneo la bahari kuu kudhibiti uvuvi haramu, leo jijini Dar es Salaam. Kulia  ni Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed akitoa zawadi kwa marubani wa ndege hiyo. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages