Serikali yatoa mil.400 kwenye matengenezo ya chumba cha upasuaji Lugoba - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Friday, 17 November 2017

Serikali yatoa mil.400 kwenye matengenezo ya chumba cha upasuaji Lugoba

Mganga Mkuu wa  halmashauri ya Chalinze ,Dkt.Rahim Hangai akizungumzia walivyojipanga kupunguza tatizo la uhaba wa upatikanaji wa huduma ya dharura za upasuaji .

Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze

SERIKALI imetoa kiasi cha sh.milioni 400 kwa ajili ya kufanyia matengenezo chumba cha dharura za upasuaji ,katika kituo cha afya Lugoba ,jimbo la Chalinze mkoani Pwani .

Kukamilika kwa kituo hicho itasaidia kupunguza adha ya kufuata huduma hiyo hospitali ya rufaa Tumbi na Bagamoyo,hasa kwa akinamama wajawazito .
 
Aidha halmashauri ya Chalinze inaendelea kuongeza vituo hivyo vya upasuaji kwa kutenga fedha za mapato yake ya ndani ,ambapo vikikamilika vitafikia vinne.

Hayo aliyasema mganga mkuu wa halmashauri ya Chalinze,Dkt.Rahim Hangai wakati alipokuwa akizungumzia namna wanavyokabiliana na changamoto ya rufaa kutokana na kukosa huduma za upasuaji wa dharura .

Alisema kipindi cha nyuma kulikuwa na tatizo kubwa hali iliyokuwa ikiwapa wakati mgumu hasa akinamama wajawazito ambao walikuwa wakikimbizwa Tumbi na Bagamoyo kufuata huduma hiyo.

Dkt.Hangai alielezea katika program ya serikali ya kuwezesha vituo 100 vitakavyotoa huduma za dharura za upasuaji ,ndipo na Chalinze imebahatika kituo cha afya Lugoba kufanyiwa matengenezo theatre ,nyumba ya mganga ,maabara .

Hata hivyo alisema kuwa ,mwezi July mwaka huu kulifunguliwa kituo kimoja cha upasuaji wa dharura Chalinze ambacho kinaleta tija kwa wananchi wanaohitaji huduma za dharura za upasuaji.

"Tunaendelea kuongeza vituo vya upasuaji kwa kutenga mapato ya ndani ili hali kutanua hospitali ya wilaya ya Msoga ambayo itakuwa na chumba cha upasuaji huo " alifafanua Dkt.Hangai .

Pamoja na hayo ,mganga mkuu huyo wa halmashauri ya Chalinze ,alieleza vikikamilika kutakuwa na vituo vinne kikiwemo Lugoba,Msoga na Chalinze .

Kingine ni kile cha Miono ambacho wamekipelekea fedha kiasi cha sh.milioni 18 .

Nae mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ,aliishukuru wizara ya afya na serikali ya awamu ya tano kwa kuwezesha kituo cha afya Lugoba kuweza kupanuliwa na kuimarisha huduma zake za afya.

Alisema Chalinze inakua siku hadi siku ,na kubeba mzigo wa watu wengine wanaotoka nje ya halmashauri wakiwemo wa ajali hivyo kunapoimarishwa huduma hizo itawasaidia wananchi .

Ridhiwani alisema huduma za afya zinahitajika kuboreshwa kwani mahitaji yamekuwa ni makubwa .

"Kwangu mimi ,tuendelee kuunga mkono juhudi za CCM na serikali kwa kuendelea kutekeleza kwa vitendo changamoto zilizokuwa zikiwakabili wananchi "

" Mwenyekit wa halmashauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu alisema wizara ya afya pia imeshatoa barua rasmi ya kuthibitisha kupandishwa hadhi kituo cha afya Msoga na kuwa hospital ya wilaya,Taarifa hizo ni faraja kwetu" alisema Ridhiwani.

Ridhiwani alisema,kwa kuwa na huduma za dharura , kuboresha hospital hiyo ya wilaya,kuboresha miundombinu ,vyoo,majengo mbalimbali ya vituo vya afya itawezesha wananchi kupata huduma bora.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages