RC Tabora: Pamba ya mkulima haitachukuliwa kwa mkopo. - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Sunday, 5 November 2017

RC Tabora: Pamba ya mkulima haitachukuliwa kwa mkopo.NA TIGANYA VINCENT
RS –TABORA

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imesema kuwa malipo kwa ajili zao la pamba yatatolewa pale pale mkulima anapouza mazao yake katika Kampuni zilizopangiwa kununua zao hilo mkoani hapo.

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri kwenye vijiji na wilaya mbalimbali wakati akihamasisha kilimo cha pamba na kuwafundisha mbinu bora za kulima kisasa kwa ajili kupata kilo nyingi kwa ekari moja.

Alisema kuwa utaratibu utakaotumika katika uuzaji na ununuzi wa pamba mkoani Tabora ni wa nipe nikupe hakuna wa njoo wiki ijayo au kesho.

Mwanri alizitaka Kampuni zote zilizopangiwa kununua pamba zikafanya maandilizi kutosha ili kuepusha usumbufu kwa wakulima kwa kukopa mazao yao.
Alisema kuwa utaratibu wa kukopa mazao ya wakulima ndio umekuwa ukisababisha wakate tamaa na kusababisha uzalishaji wa zao hilo kudhofika, lakini wakilipwa palepale wakulima watapata hamasa na kulima kwa wingi zaidi katika msimu unaofuata.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alitoa wito kwa watu waliojitokeza kulima zao hilo kuzingatia kanuni na sheria za kilimo cha zao hilo kwa kuepuka kuweka uchafu na kumwagia maji pamba yao ili waweze kupata bei nzuri.

Alisema kuwa mtu atakayebainika kuchafu pamba kwa lengo la kufanya udanganyifu atachukuliwa hatua kali kulingana na sheria inayoongoza zao hilo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa huyo amesisitiza Kampuni zote zinazosambaza pembejeo kwa wakulima wa pamba kuhakikisha bidhaa hizo zinawafikisha wakulima kabla ya mwisho wa wiki ijayo ili waweze kwenda sanjari na msimu wa kilimo.

Alisema kuwa zaidi ya hapo watasababisha wakulima washindwe kuzalisha kwa wingi na kupata mafanikio kidogo.

Naye Diwani wa kutoka Kata ya Lutende wilayani Uyui Pancras Ruge alisema kuwa kuja kwa zao la pamba kutawasaidia wakazi wa maeneo hayo kwani walikuwa hawana zao lolote la biashara.

Aliomba mbegu ziwahi kufika katika maeneo yote ambayo wakulima wamejiandikisha kwa ajili ya kulima zao hilo na kuongeza kuwa watazingatia elimu iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa ili waweze kuzalisha kilo 1000 hadi 1200 katika ekari moja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages