Habari za sasa hivi

Rais Robert Mugabe ajitokeza hadharani kwa mara ya kwanza

 Rais Robert Mugabe amejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza hii leo tangu jeshi litwae udhibiti wa nchi hiyo siku ya jumatano.Rais Mugabe ameonekana akihudhuria mahafali ya Chuo Kikuu Huria Jijini Harare ambacho yeye ni mkuu wa chuo.Rais Mugabe amekuwa akishikiliwa nyumbani kwake kwa siku kadhaa, baada ya jeshi kuamua kuingia mtaani kufuatia mgogoro wa kumtimua makamu wa rais.
Rais Robert Mugabe akiwa katika mahafali ya Chuo Kikuu Huria Harare, hata hivyo yaonekana hana ratiba ya kuhutubia