Header Ads


Maafisa wa Jeshi la Polisi kikosi cha Reli mtandao wa Polisi wanawake Dawati la jinsia wamewatembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

 Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha Reli Koplo Grace Ndyamukama akimjulia hali mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Taasisi hiyo leo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia. Kulia ni Mama wa mtoto Nasra Khalfan.
 Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) ambaye pia ni Mkuu wa kituo cha Polisi Reli Martha Mdinka akimpa zawadi ya dawa ya meno, maji ya kunywa na juisi  Hadija Selemani ambaye amelazwa na mtoto katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Taasisi hiyo leo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia.
 Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha Reli Rhoda Israel  akimpa zawadi ya juisi  Sada Issah ambaye amelazwa na mtoto katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Taasisi hiyo leo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia.
  Maafisa wa  Jeshi la Polisi kikosi cha Reli wakigawa zawadi za maji ya kunywa, dawa za mENO,  juisi, mafuta ya kupakaa, sabuni za kuogea na kufulia kwa watoto waliolazwa  katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia.
 Maafisa wa  Jeshi la Polisi kikosi cha Reli wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kutembelea Taasisii ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kugawa zawadi za maji ya kunywa, dawa za meno,  juisi, mafuta ya kupakaa, sabuni za kuogea  na kufulia kwa watoto waliolazwa  katika taasisi hiyo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia.
 Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha Reli Jane John akimpa zawadi za maji ya kunywa, dawa ya meno,  juisi, mafuta ya kupakaa na  sabuni Maimuna Daud  ambaye amelazwa na mtoto katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea Taasisi hiyo leo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) ambaye pia ni Mkuu wa kituo cha Polisi Reli Martha Mdinka akiongea jambo na wagonjwa walipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  leo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mtandao wa Polisi  Wanawake Dawati la Jinsia.

Picha na JKCI
ASKARI wa Jeshi la Polisi kikosi cha Reli mtandao wa Polisi wanawake Dawati la jinsia wamewatembelea na kuwagawia zawadi mbalimbali watoto waliolazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa ajili ya matibabu ya moyo.

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo ,  Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) ambaye pia ni Mkuu wa kituo cha Polisi Reli Martha Mdinka alisema wamewatembelea wagonjwa hao ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.

“Tumekuja kuwatembelea na kuwagawia vitu mbalimbali ikiwamo sabuni za kuogea na kufulia, dawa za meno, maji ya kunywa, juisi na vitu vingine ambavyo vyote vina thamani ya zaidi ya shilingi laki nne,” alisema.

ASP Mdinka aliongeza pia  kutembelea Taasisi hiyo kumewapa   nafasi ya kumtembelea na kumsalimia mtoto Salome ambaye amelazwa hospitalini hapo kwa ajili ya  kutibiwa ugonjwa wa moyo.

“Salome tulimpokea katika kituo cha Reli tukamleta hapa JKCI kwa ajili ya matibabu lakini familia imemtelekeza licha ya kwamba ametibiwa na anaendelea vizuri,” alisema.
Aliongeza “Bado yupo hapa hospitalini, tunaendelea kushirikiana kwa ukaribu na vyombo vingine ili kuhakikisha anapata sehemu ya kujisitiri ili aweze kuendelea na maisha yake kama watoto wengine, apate haki zake za msingi ikiwamo elimu,”.
Post a Comment
Powered by Blogger.