Katibu Mkuu Suhaba Nkinga: wataalam wa maendeleo ya jamii ni wakala wa kufikia maendeleo ya uchumi wa viwanda. - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Thursday, 9 November 2017

Katibu Mkuu Suhaba Nkinga: wataalam wa maendeleo ya jamii ni wakala wa kufikia maendeleo ya uchumi wa viwanda.

 Katibu Mkuu maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga akizungumza na maafisa Maendeleo ya Jamii na kuwaasa kuamsha ari ya wananchi kushiriki kazi za maendeleo katika siku ya tatu ya Mkutano wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unaofanyika Ukumbi cha Chuo cha Mipango mjini Dodoma.
 Afisa kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Bakari George akitoa mada kuhusu namna bora ya Maafisa Maendeleo ya Jamii kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo kuelekea Uchumi wa Viwanda wakati wa siku ya tatu ya Mkutano wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unaofanyika Ukumbi cha Chuo cha Mipango mjini Dodoma.
 Mratibu wa Masuala ya Maendeleo ya Jamii kutoka OR TAMISEMI Bi. Mwajina Lipinga OR-TAMISEMI akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Uratibu, Ufuatiliaji na Tathimini ya Shughuli za maendeleo ya Jamii katika Secretarieti za Mikoa na halmashauri za mitaa, wakati wa siku ya tatu ya Mkutano wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unaofanyika katika Ukumbi cha Chuo cha Mipango mjini Dodoma.
 Maafisa Maendeleo ya Jamii wakijadiliana katika vikundi vya kikanda kuhusu namna bora ya kuamsha ari na kuwashirikisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo katika ngazi ya jamii katika siku ya tatu Mkutano wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unaofanyika katika Ukumbi cha Mipango mjini Dodoma.
Mwakilishi wa Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Kanda ya Ziwa Bw. Lawi Msahi akiwasilisha mapendekezo ya kikundi  kuhusu namna bora ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo kwa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(hayupo pichani) wakati wa siku ya tatu ya Mkutano wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unaoendelea katika Ukumbi cha Chuo cha Mipango mjini Dodoma.
Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Wataalam wa Sekta ya maendeleo ya Jamii wameshauriwa kuwa mawakala wa wananchi katika kuamsha ari, hamasa na raghiba ya kufikia uchumi wa viwanda.

Ushauri huo umetolewa mjini Dodoma na Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga alipokuwa akiongoza mjadala wa siku ya tatu ya Mkutano wa kazi wa Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii unaofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.

BIbi. Sihaba Nkinga amesema kuwa wataalamu wa maendeleo ya jamii wanajukumu la kuchechemua ari ya wananchi kubadili fikra zao ili kuwa tayari kushiriki azma ya uanzishaji wa viwanda mbalimbali vitakavyo changia kukuza ustawi wa watu na kusisimua ukuaji wa uchumi na maendeleo ya Taifa.

Aidha ameeleza kuwa, kampeni ya kuamsha ari ya kila mwananchi kuchangia shughuli za maendeleo kuelekea kuwa na uchumi wa kati na viwanda wataalam wa maendeleo ya jamii ni chachu ya uanzishaji wa shughuli za uzalishaji mali na uwekezaji katika sekta ya viwanda, kuibulia kwa miradi inayomilikiwa na wananchi wenyewe ili kukuza kipato na kulinda dhidi ya vitendo ukatili wa kijinsia.

“Tutafute mbinu wezeshi na sahihi za kuasha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo katika maeneo yao kuelekea Uchumi wa Viwanda” alisema Bibi. Sihaba.
  
Akitoa mada katika mkutano huo, Mchumi Mkuu kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw.Exaud Kigahe amesema anatambua kuwa jukumu la watalaam wa maendeleo ya jamii katika kuhakikisha kuwa wananchi wanajengewa uelewa na hamasa ya kuchochea uanzishaji wa viwanda vidogo na vya kati vitakavyochakata malighafi zilizopo katika mazingira yao na kusisimua ukuaji wa pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 40, na ongezeko la ajira kwa zaidi ya asilimia 40.

Amesisitiza kuwa mchango huo wa wataalamu wa Maendeleo ya jamii utawezesha wananchi kutambua lengo mahususi la uanzishaji wa viwanda, thamani ya kuzalisha bidhaa zenye ubora, na matumizi ya teknolojia rahisi na sahihi katika kusisimua ukuaji wa uchumi na viwanda ili kufikia maendeleo jumushi ya taifa.

“Watalaamu wa maendeleo ya jamii wanasifa kuu ya kwenda kwa watu, kuishi na watu, kujifunza kutoka kwao, na kupanga pamoja kushawishi mabadiliko ya kweli kuanzia pale walipo”. Alisema Bw. Kigahe.   

 Maafisa Maendeleo ya Jamii nchini watasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha mkakati wa Taifa la viwanda, kwa kujitambua kuwa wanadhana na uwakala wa mabadiliko katika jamii katika kuraghibisha jamii kuitikia uanzishaji wa viwanda vitakavyosaidia nchi kuelekea Uchumi wa kati na wa Viwanda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages