Hatua kali kuchukuliwa kwa kampuni za kusambaza pembejeo itayakomsababisha mkulima kupata hasara - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Thursday, 2 November 2017

Hatua kali kuchukuliwa kwa kampuni za kusambaza pembejeo itayakomsababisha mkulima kupata hasara

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imetoa onyo kwa Kampuni zote za usambazaji pembejeo za zao la Pamba kuhakikisha mbegu na dawa za kuua wadudu watakazopeleka kwa wakulima ni bora na hazina matatizo ili zisije zikawasababishia hasara wakulima.

Onyo hilo limetolewa jana wilayani Nzega na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa mkutano wa kuwaelimisha wakulima juu ya kulima zao hilo kwa kufuata Sheria na Taratibu zake ili kuongeza ubora.

Alisema kuwa Kampuni hizo zilizopewa kazi ya kusambaza Mbegu kwa wakulima wa pamba katika Wilaya Tano za Mkoa huo ni vema zikapeleka mbegu bora na zilizopendekezwa kulima zao hilo ni vema zikahakikisha kuwa zinapeleka kwa wakulima mbegu iliyopendekezwa ya UKM08 ambayo iko katika ubora na wakawa na uhakika kuwa inatoa ili kuwaepusha wakulima kupoteza nguvu zao.

Mwanri aliongeza kuwa na ni vema wakahakikisha dawa watakazosambaza kwa wakulima wa Pamba katika maeneo ya Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kuua wadudu zikawa ni zile zilizopendekezwa na zina uwezo kweli wa kuua wadudu haribifu na kuongeza kuwa kinyume cha hapa atawakamata wao na wali zao ili waweze kufidia hasara kwa mkulima.

“Najua nyie Kampuni zilizopewa jukumu la kusamabaza mbegu kwa wakulima na dawa mtapeleka mbegu bora na zilizokubalika…ikitokea kuwa mbegu mlisambaza kwa wakulima zikashindwa kuota na dawa ikashindwa kuua wadudu…mimi nitakachofanya ni kukamata mali zenu zote ili ziuzwe kufidia hasara ambayo wakulima watakuwa wamepata “ alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Alisema kuwa yeye kama Mkuu wa Mkoa anabeba dhamana ya kuhakikisha kuwa hakuna mkulima yoyote anapata hasara kwa sababu za makusudi au uzembe wa watendaji wowote wale bali yuko pale kuwashika mkono wakulima.

Kwa upande wa Meneja  kutoka Kampuni ya Quton Tanzania limited iliyozalisha Mbegu zinazosambazwa katika maeneo mbalimbali Phineas Chikaura alisema kuwa mbegu hiyo inasambazwa katika maeneo mbalimbali katika Wilaya yaNzega inao ubora ambao umedhibitishwa na Taasisi ya utafiti wa Mbegu hapa nchini.

Alisema kuwa kinachotakiwa kwa mkulima wa pamba ni pamoja na kufuata kanuni za upandaji wake ikiwa ni pamoja na shimo kutozidi urefu wa sentimeta tatu na mbegu kutolowekwa kama baadhi wanavyofanya.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa ameziagiza Kampuni hizo zinazosambaza Mbegu kahakikisha Mbegu na vifaa vyote vinavyotakiwa kwa mkulima kuanza kupanda vinafika kwa mkulima ndani ya siku 10 zijazo.

Alisema kuwa nje ya hapo mvua zikianza kunyesha upo uwezekana wa mbegu kuchelewa kumfikia mkulima na hivyo kushindwa kulima na kumkatisha tamaa.

Mwanri aliwaagiza Maafisa Ugani wote kuhakikisha wanajipanga vizuri ili kufuatilia kama kweli wakulima wote wamepata mbegu kwa wakati.

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa amepiga marufuku mizani ya rula kutumika wakati wa zoezi la ununuzi wa pamba katika enro hilo badala yake alisema kuwa utakaokuwa unatumika ni ule wa dijitali.

Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuondoa wizi ambao wakulima wamekuwa wakifanyiwa kupitia mizani ya rura na kuwafanya kupata mapato kidogo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora yuko katika ziara ya kutembelea wilaya zote zinazolima Pamba ambazo ni Igunga, Nzega, Uyui, Urambao na Kaliua kuwahamasisha wakulima kulima kilimo cha kisasa na kuondokana na tabia ya kuchafua pamba ili waweze kupata bei nzuri

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages