ACACIA bulyanhulu wakabidhi maktaba ya kisasa Wilaya ya Nyang'hwale yenye thamani ya milioni 23 - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Sunday, 26 November 2017

ACACIA bulyanhulu wakabidhi maktaba ya kisasa Wilaya ya Nyang'hwale yenye thamani ya milioni 23

Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Bernedict Busunzu akipatiwa maelezo na mkurugenzi wa Read International ,Bi Magdalena George wakati walipokuwa wakitembelea maktaba ya jamii ambayo hipo wilayani Nyang’hwale ,katika kati ni katibu tawala wa Wilaya hiyo Fabian Sospeter.

Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Bernedict Busunzu akikata utepe na katibu tawala wa Wilaya ya Nyang’hwale Bw,Fabian Sospeter wakati wa zoezi la kukabidhi maktaba hiyo.

Sehemu ya vitabu ndani ya maktaba ya jamii wilayani Humo.

Sehemu ya vitabu ndani ya maktaba ya jamii wilayani Humo.

Meneja Ufanisi wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu,Bw Elias Kasititila akielezea namna ambavyo wameguswa kuchangia maktaba hiyo.

Bi,Vannesa Kasoga akisoma taarifa ya ukamilikaji wa maktaba hiyo tangu ilipoanza kufanyiwa maboresho na kampuni ya ACACIA.

Mkurugenzi wa Read International ,Bi Magdalena George akielezea namna ambavyo wameweza kufanukisha kuhakikisha maktaba inakuwa kwenye muonekano bora.

Katibu tawala wa Wilaya ya Nyang’hwale Bw,Fabian Sospeter akiwasisitiza wananchi pamoja na wanafunzi kutumia maktaba hiyo kujifunza mambo mbali mbali.
Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Bernedict Busunzu akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi wakati wa zoezi la kukabidhi na kuzindua maktaba ya jamii wilayani Nyang’hwale.
Wananchi ambao wamejitokeza kwenye zoezi la uzinduzi wa Maktaba.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Karumwa wakiwa kwenye uzinduzi wa maktaba ya jamii.

Na,Joel Maduka.


Mgodi wa acacia Bulyanhulu kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la  read international wamekabidhi maktaba ya kisasa ya jamii ambayo imetumia kiasi cha sh,milioni 23  hadi kukamilika kwake  kwa halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale ambayo itawasaidia wananchi kupata maarifa na kujifunza mambo mbali mbali kutokana na vitabu ambavyo vinapatikana.
  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages