Shule ya sekondari lugoba yakabiliwa na upungufu wa madarasa sita na ukosefu wa uzio - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Sunday, 22 October 2017

Shule ya sekondari lugoba yakabiliwa na upungufu wa madarasa sita na ukosefu wa uzio

Mwalimu mkuu shule ya sekondari Lugoba, alhaj Abdallah Sakasa akizungumza jambo na wanafunzi na wazazi wa wanafunzi shuleni hapo (hawapo pichani ).

(Picha na Mwamvua Mwinyi )

Na Mwamvua Mwinyi,Lugoba

SHULE ya sekondari ya Lugoba iliyopo Lugoba, Chalinze, Bagamoyo mkoani Pwani, inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa sita na ukosefu wa uzio.

Upungufu huo unatokana na wingi wa wanafunzi wanaojiunga na masomo shuleni hapo kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo ,alhaj Abdallah Sakasa ameeleza shule ya sekondari Lugoba ilianzishwa miaka 28 iliyopita , ambapo kuna uchakavu kwenye baadhi ya vyumba vya madarasa .

Hata hivyo ,amesema zipo jitihada zinazochukuliwa kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo shule hapo ikiwemo viongozi wa serikali, halmashauri na mlezi wao Subhash Patel, kushirikiana kutatua tatizo hilo.

Alhaj Sakasa amewaomba wadau mbalimbali wa elimu kujitokeza kushirikiana kutatua changamoto hizo ili kuinua taaluma kwa wanafunzi .

Diwani wa Kata ya Lugoba Rehema Mwene, amesema halmashauri imechukua hatua za kupambana na upungufu wa vyumba vya madarasa na katika bajeti ya msimu huu imetenga sh.mil. 10 kwa ajili ya kupunguza changamoto hiyo.

Shule ya sekondari Lugoba ,ilianzishwa mwaka 1989 kwa sasa ina wanafunzi 1,353 kati yao wavulana 721, wasichana 632.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages