RC Tabora chagueni vipaumbele vichche vya kuanza navyo katika utekelezaji wa miradi ya wananchi. - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Sunday, 29 October 2017

RC Tabora chagueni vipaumbele vichche vya kuanza navyo katika utekelezaji wa miradi ya wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri .
..
NA TIGANYA VINCENT RS-TABORA
UONGOZI wa Halmashauri zote za mkoani Tabora umetakiwa kuchagua vipaumbele vichache vya miradi  itakayoanza navyo kuitekeleza  ili iweze kutekezwa kwa kiwango cha juu na unafisi na hivyo kuwa na tija ambayo itawanufaisha wananchi wengi badala ya kunufaisha wachache.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya Madiwani wa Halmashauri ya Kaliua na Wakuu wa Idara yanayoendeshwa na wakufunzi kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo.

Alisema kuwa ni vema madiwani kwa umoja wao wakaa pamoja na kuangalia miradi michache ambayo inaweza kunufaisha Kata nyinyi au wananchi na kuachana na ubinafsi ambao kila Diwani anataka mradi uanzie kwake na kujikuta wakichelewa kutoa maamuzi.

Mwanri alisema kuwa ubifasi huo unasababisha mara nyingi miradi kutekelezwa nusu nusu na hivyo kutokuwa msaada wa kuwaletea wananchi maendeleo.

Alisema kuwa katika kuchagua miradi ni vema wakaangalia malengo mapana ya miradi ili waweze kufikia maamuzi yatakayoleta tija na kusaidia kuwaondolea wananchi matatizo.

Mwanri alisema kwa kuwa fedha ni kidogo ni vema madiwani wakawa na umoja katika kuchagua miradi ya kuanzia na itakayofuatia kwa kuangalia maslahi mapana ya Halmashauri zao na wananchi wanaowahudumia.

“Miradi mingi inafanyika kwa kitu kinachoitwa kipaumbe …ukienda katika na kukuta kila Diwani anavutia kwake katika mradi ambao ungejengwa katika Kata moja na kunufaisha wengi …ujue hawa wananchi watachelewa kupata maendeleo…ni vema wakawa kitu kimoja katika kuchagua vipaumbele” alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kaliua John Pima alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Madiwani na Wakuu wa Idara watoe maamuzi mazuri ambayo yatasaidia kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi.

Alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuboresha mahusiano na usimamizi kati ya madiwani na wakuu wa Idara ili kuhakikisha shughuli za Halmashauri inakwenda vizuri.

Pima alisema kuwa hivi sasa wanalenga kuhakikisha kuwa wanaibua miradi ya kijamii , hivyo miradi ya kijamii haiwezi kwenda vizuri kama Madiwani hawatajua wanatakiwa wasimamie nini.

Alisema kuwa mafunzo yatawajengea uwezo wakuu wa Idara na madiwani ili waweze kujua kuwa miradi inaibuliwa ni muhumu katika eneo hilo na itakuwa endelevu kwa jamii husika na isaidie kutatua kero na matatizo yao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kuwafanya waende na wakati ili waweze kuisimamia na kuongoza Halmashauri kwa ajili ya kuongeza mapato na kuleta maendeleo kwa wananchi.

Alisema kuwa mafunzo yatasaidia kuwafanya Wakuu wa Idara, Madiwani na Viongozi wa Wilaya kuwa timu moja katika kusaidia wananchi kuondokana na umaskini.

Kwa upande wa Mhadhiri kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Eliakundi Samanga alisema kuwa wanatoa mafunzo kwa Madiwani hao na wakuu wa Idara ili kujwajengea uwezo wa kuweza kutoa huduma kwa wananchi kwa ubora na ufanisi zaidi.

Alisema kuwa watawafundisha yatawasidia kujengea uwelewa wa pamoja kati ya Madiwani na Wakuu wa Idara ili kutoa huduma kwa jamii kwa ufanisi mkubwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages