RC Ndikilo-Pwani bado inapambana na viashiria vya kiuhalifu - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Tuesday, 31 October 2017

RC Ndikilo-Pwani bado inapambana na viashiria vya kiuhalifu

MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,akizungumza na viongozi wa kamati za ulinzi na usalama mkoa wa Lindi,Mtwara na Ruvuma huku mkoa wa Pwani ukiwa mkoa mwenyeji huko Bagamoyo (hawapo pichani),wakati walipokutana kujadiliana na kubadilishana uzoefu katika masuala ya ulinzi na usalama.

(Picha na Mwamvua Mwinyi)
..
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo

MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo,amesema mkoa huo bado unaendelea na oparesheni na misako mbalimbali ili kupambana na viashiria vya uhalifu vinavyoweza kuhatarisha amani mkoani humo.

Aidha amesema katika oparesheni hiyo inayoendela wapo baadhi ya watuhumiwa wa kiuhalifu ambao wamekamatwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Kutokana na hilo,amezitaka kamati za ulinzi na usalama mkoa wa Lindi,Mtwara na Ruvuma kuangalia kwa pamoja viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyoweza kuikumba mikoa hiyo.

Akizungumza na viongozi wa kamati za ulinzi na usalama za mikoa hiyo mitatu huku mkoa wa Pwani ukiwa ni mkoa mwenyeji huko wilayani Bagamoyo,mhandisi Ndikilo ,alieleza dhamana waliyopewa ni kulinda watu na mali zao .

Alielezea ,kukutana kwao iwe chachu ya kuchukua hatua madhubuti ndani ya mikoa yao ili hali wananchi wafanye shughuli zao za kuwaongezea kipato kwa usalama  bila hofu .

Pamoja na hayo ,mhandisi Ndikilo alisema kwamba,kikao hicho kitasaidia kubadilishana uzoefu mbalimbali kwenye mbinu za kiitelijensia na namna ya kuendesha oparesheni mbalimbali za kupambana na wahalifu.

“Sisi mkoani kwetu tuliendesha oparesheni kali sana baada ya wilaya zetu tatu za Mkuranga ,Kibiti na Rufiji kukumbwa na uhalifu na mauaji yaliyosababisha vifo vya raia na polisi ,”

“Tunaendelea na oparesheni hiyo na vijana wetu hawalali usiku na mchana,tunaendelea kuwasaka wahalifu wachache wanaotaka kuondoa amani tuliyonayo ,”‘Hivyo kutokana na hilo naamini mtajifunza mengi kutoka kwetu" 

“”,Na sisi tutajifunza mengi kwenu ikiwemo uzoefu misako mnayoiendesha na mbinu mnazozitumia ,”Naamini kubadilishana uzoefu itasaidia mikoa yetu  kuishi kwa amani na utulivu na kuondoa wahalifu wasiotutakia mema “alisema mhandisi Ndikilo.

Mhandisi Ndikilo,alisema dhamira ya kuwa na viwanda na kukuza uchumi na uwekezaji ndani ya mikoa haiwezi kutimia endapo kuna uvunjifu wa amani .

Aliiomba jamii ishirikiane kufichua wahalifu na wananchi waungane na dola kudhibiti vitendo vya kiuhalifu,unyang”anyi na ujambazi kwenye maeneo yao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages