Mgalu-awataka wakandarasi wanaotekeleza mradi wa rea wawe kwenye maeneo yao ya kazi - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Tuesday, 17 October 2017

Mgalu-awataka wakandarasi wanaotekeleza mradi wa rea wawe kwenye maeneo yao ya kazi

Naibu waziri wa nishati ,ambae pia ni mbunge viti maalum Mkoani Pwani ,Subira Mgalu ,akionekana picha akizungumza wakati alipokuwa,huko Lugoba jimbo la Chalinze.

(Picha na Mwamvua Mwinyi)
...
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze

WAKANDARASI wanaotekeleza mradi wa usambazaji wa umeme vijijini,(REA)awamu ya Tatu ,wametakiwa kuwa kwenye maeneo yao ya kazi ili kufanikisha mradi huo kwa wakati na kuleta matumaini ya umeme kwa wananchi ambao bado hawajafikiwa.

Naibu waziri wa nishati ambae pia ni mbunge wa viti maalum mkoani Pwani Subira Mgalu ,aliyasema hayo ,Lugoba huko Chalinze mkoani Pwani .

Alisema anaanza ziara kupitia maeneo yao ya kazi na ataendelea kusimamia ili mradi huo ulete tija kwa watanzania hadi vijijini .

Subira alitoa rai kwa wakandarasi hao kutekeleza majukumu yao kwa wakati kwa kuzingatia uhitaji wa huduma ya umeme nchini kwa lengo la kutimiza azma ya serikali ya kuwa nchi ya viwanda.

Aidha alieleza ,wizara hiyo imeamua vifaa vyote vya umeme vitaanza kutengenezwa nchini ikiwemo nguzo,transformer,mita ili shirika la umeme nchini(Tanesco)lisiwe na visingizio vingi vya kutounganishia umeme kwa wateja wapya .

Alisema yapo maombi  mengi lakini yanachukua muda mrefu kufanyiwa utekelezaji ,yakiwepo maombi yaliyokaa miezi sita hadi mwaka .

Subira alieleza ,wizara imeshakaa na wadau mbalimbali wa uzalishaji vifaa hivyo na wameonyesha utayari wa kufanikisha hatua hiyo .

"Ni vyema vifaa hivi muhimu vikapatikana nchini kuliko kuvitoa nje ya nchi suala linalosababisha visingizio vingi na kukwamisha jitihada za kuunganisha umeme kwa wateja wengi " alisisitiza Subira .

Pamoja na hayo alisema ,Tanesco wawe vizuri kutoa taarifa ya kukatika kwa umeme mapema kwa wananchi ili kuwaondolea usumbufu na kulinda vifaa vyao .

Naibu waziri huyo wa nishati alisema kwamba,yapo maeneo umeme unashida ,unakatikakatika bila taarifa .

Subira alisema ,waziri Wa Nishati Dkt Medard Kalemani ,ameshampatia majukumu ya kuanza kuyasimamia ikiwemo mradi huo,unaotekelezwa na (REA) awamu ya tatu kwa kushirikiana na Tanesco,utakao sambaza umeme kwa vijiji vyote ambavyo havikupata huduma hiyo wakati wa REA awamu zilizopita .

Alisema kuwa, REA awamu ya tatu itatekelezwa kwa miaka mitano hadi kufikia 2021.

“, Ninatambua kuna maeneo awamu ya kwanza na ya pili hayajaunganishiwa ,mengine yamerukwa ,mradi huu sasa utamaliza kazi ya kuunganisha huduma ya umeme katika vijiji vyote 7,587 nchini vilivyoachwa ili kufikia idadi ya vijiji vyote 12,262,Tanzania bara ifikapo mwaka 2021”, alisema Subira .

Hata hivyo ,Subira alielezea serikali imejipanga kutekeleza miradi yote ya kuzalisha umeme ikiwa ni sanjali na ule wa stiegler's gauge uliopo Rufiji ambao utazalisha megawatts 2,100.

Mradi mwingine ni wa Kinyerezi I na Kinyerezi II na mingine ili kufikia malengo ya nishati hiyo kufikia watanzania Wa mjini na vijijini nchini.

Kwa upande wake ,mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete alimpongeza Subira kwa kuteuliwa kuwa Naibu waziri wa nishati na kumuomba kufuatilia maeneo ambayo hajafikiwa na REA Chalinze .

Alisema yapo maeneo yamerukwa na umeme hivyo anaamini awamu ya tatu itatoa kipaombele katika maeneo hayo .

Ridhiwani ,alivitaka vijiji ambavyo havijafikiwa Chalinze kuvuta subira kwani mradi huo ni wa awamu na hakuna maendeleo yasiyo na hatua .

Mbunge huyo ,alisema ataendelea kusimamia changamoto ya ukosefu wa umeme kwenye baadhi ya maeneo .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages