RC Makonda atembelea na kukagua daraja lililoharibika Mbezi Kibanda cha Mkaa - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Sunday, 29 October 2017

RC Makonda atembelea na kukagua daraja lililoharibika Mbezi Kibanda cha Mkaa

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es  Salaam Mheshimiwa Paul Makonda ametembelea na kukagua daraja lililoharibika juzi Alhamisi kutokana na kunyesha mvua kubwa katika eneo la  Mbezi Kibanda cha Mkaa jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo ameifanya leo tarehe 28 Oktoba 2017 akiwa katika muendelezo wa ziara ya kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na mvua inayoendelea kunyesha  jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mh. Makonda aliwataka wakazi wa Dar es Salaam kutokubaki katika mazingira hatarishi  sambamba na kutokuchimba mchanga, na kutokutupa taka kwenye mito.

"Nawaasa wananchi wa jiji la Dar es Salaam  kuchukua tahadhari mapema kwani wataalamu wa hali ya hewa wanasema tarehe 1  November  2017 kuna mvua kubwa zaidi itakuja kuliko tuliyoiona kwa hiyo tuache kuchimba mchanga kwenye mito, tuhame kwenye mabonde na tuache kuchafua mito yetu kwani tusipofanya hivyo yatatokea madhara makubwa" alisema Makonda.

Pia Mh. Makonda alisema kuna ujenzi wa barabara unakuja mpaka Chalinze na Tanroad washafanya upembuzi yakinifu na wako mbioni kuanza ujenzi huo.

Mwisho Mh. Makonda aliwasihi wananchi  wachukue tahadhari mapema ili kuepuka maafa yasiyo ya lazima yatakayosababishwa na mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha kuanzia tarehe moja ya mwezi ujao.

*IMETOLEWA NA*
*KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO*
*HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO*

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages