Header Ads


Madaktari india wafanikiwa kutenganisha mapacha walioungana vichwa

 Madaktari bingwa wa upasuaji nchini India katika Jiji la Delhi wamefanikiwa kuwatenganisha watoto mapacha walioungana vichwa.

Watoto hao wa mwaka mmoja waitwao Jaga na Kalia wamefanyiwa upasuaji kwa muda wa saa 16, na kwa sasa wapo kwenye chumba cha wagonjwa mahututi, kwa mujibu wa madaktari.

Timu ya madaktari 30 waliofanya upasuaji huo wote wanatoka Taasisi ya Sayansi ya Tiba ya nchini India.

Watoto hao mapacha wanaume walizaliwa wakiwa wamechangia mishipa ya damu na mishipa midogo ya kwenye ubongo.
 Mmoja wa watoto mapacha walioungana kichwani akiwa amelala baada ya kutenganishwa
Post a Comment
Powered by Blogger.