Koka atoa vyerehani vinne kwa shirikisho la watu wenye ulemavu Kibaha - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Tuesday, 17 October 2017

Koka atoa vyerehani vinne kwa shirikisho la watu wenye ulemavu Kibaha

katibu wa Mbunge wa Kibaha Mjini ,Method Mselewa alievaa miwani juu ya kichwa ,akifurahi mara baada ya kukabidhi vyerehani vinne kwa shirikisho la watu wenye ulemavu -Kibaha.(Picha na Mwamvua Mwinyi )

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha mkoani Pwani, Silvestry Koka ametoa vyerehani vinne kwa shirikisho la watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) wilayani Kibaha ili waweze kujishughulisha na kujiongezea kipato .

Aidha Koka ,ameelezea kwamba ataendelea kuwezesha makundi yote maalum bila kubagua ikiwemo vijana,wanawake ,wazee na wenye ulemavu .

Akikabidhi vyerehani hivyo kwa uongozi wa shirikisho hilo ,katibu wa Mbunge huyo Method Mselewa alisema ,Koka ametimiza ombi la shirikisho hilo. 

Alieleza watu wenye ulemavu nao wanapaswa kusaidiwa kama wanavyosaidiwa wengine wasio na ulemavu ili kujiendeleza kimaendeleo na kiuchumi.

“Watu wenye ulemavu wapo wanaoweza kufanya kazi ,ujasiriamali kama wengine ,ulemavu siyo mwisho wa maisha "

"Nguvu mnazo na mnao uwezo kama watu wasiokuwa na ulemavu na tutaendelea kuwasaidia ili nanyi mjikwamue kwa kujiongezea kipato,” alisema Mselewa.
Mselewa alisema kuwa kutokana na shirikisho hilo kuungana kutasaidia kuwafikia kwa urahisi kuliko kuwa binafsi ingekuwa ngumu.

“Hizi mashine mnapaswa kuzitunza ,na mjue mbali ya kuwapatia ujuzi, zitawaingizia fedha ambazo zitaweza kuwafanya muwe na mapato kuliko kuomba jambo ambalo halifurahishi,” alisema Mselewa.

Nae mwenyekiti wa SHIVYAWATA, Ally Mlanga alishukuru msaada huo na kusema huo ni kama mtaji ambao watahakikisha wnaauendeleza.

Mlanga alielezea ,hawataki fedha ila wanachotaka ni kupewa vitu ama msaada utakaowasaidia kuliko fedha ambazo zinaweza kutumika vibaya na kupotea kwa urahisi.

Kwa upande wake ,Afisa Maendeleo wa Kata ya Kibaha ,Regina Lazaro alisema kupatiwa vyerehani hivyo vitawasaidia kujiongezea kipato kwani moja ya shughuli zake ni kuhamasisha ujasiriamali.

Alisema kuwa ,wamekuwa wakishirikiana na shirikisho hilo ikiwa ni njia mojawapo ya kuwasaidia kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na serikali ama wadau toka sekta binafsi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages