Jumla ya watahiniwa 9346 Mkoani Tabora kufanya mitihani ya kidato cha nne mwaka huu(2017). - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Sunday, 29 October 2017

Jumla ya watahiniwa 9346 Mkoani Tabora kufanya mitihani ya kidato cha nne mwaka huu(2017).

NA TIGANYA VINCENT RS-TABORA
JUMLA ya watahiniwa 9346 mkoani Tabora wamesajiliwa kufanya mitihani ya Kidato cha Nne mwaka huu(2017).

Watahiniwa hao wanatoka Shule za Sekondari 173 ambapo kati ya hizo 153 ni za Serikali na 20 ni shule binafsi.

Takwimu hizo zimetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari alikuwa akizungumzia maandalizi ya jumla ya zoezi la kuanza mitihani.

Alisema kuwa watahiniwa hao 7,714 ni wa shule na 1,632 ni wale kujitegemea na kuongeza kuwa kutakuwepo na watahiniwa wa mtihani wa maarifa (QT)401 .

Mwanri aliwataka wasimamizi na watahiniwa wote kujiepusha na vitendo vya udanganyifu wa aina yoyote na kuagiza Kamati zote zihakikishe ulinzi na usalama wa mitihani unakuwa madhubuti katika kipindi chote.

Alisema kuwa Serikali haitasita kumchukua hatua kali yoyote atakayebainika udanganyifu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages