Header Ads


Bondia Athony Joshua atetea mikanda yake ya WBA na IBF

 Bondia Anthony Joshua akimshindilia ngumi ya kulia bondia Carlos Takam
 Anthony Joshua akimshindilia ngumi nzito Carlos Takam katika pambano hilo
 Bondia Carlos Takam akianguka chini baada ya kushindiliwa ngumi na Anthony Joshua
 Refa Phil Edwards akiingilia kati na kusimamisha pambano baada ya Takam kuzidiwa
Bondia Anthony Joshua ametetea mikanda yake ya uzito wa juu ya WBA na IBF baada ya kuibuka na ushindi kufuatia refa kusitisha kiutata pambano hilo katika raundi ya 10 dhidi ya Carlos Takam.

Katika pambano hilo Muingereza Joshua, 28, aliumia pua yake baada ya kugongana kwa nguvu kwa kichwa na Takam mapema katika pambano hilo na bondia huyo ambaye aliyejiandaa kwa pambano hilo kwa siku 12.

Takam ilibidi achunguzwe mara mbili na madaktari kutokana na kipigo kabla ya kuzidiwa zaidi katika raundi ya 10 pale refa Phil Edwards alipoingilia kati kusimamisha pambano hilo hatua ambayo haikuwafurahisha mashabiki na kuzomea.
Post a Comment
Powered by Blogger.