CCM Bagamoyo kuunda baraza la wazee makada - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Thursday, 19 October 2017

CCM Bagamoyo kuunda baraza la wazee makada

MWENYEKITI mpya wa chama cha mapinduzi (CCM)wilayani Bagamoyo,mkoani Pwani,alhaj Abdul Sharif akizungumza na baadhi ya viongozi mbalimbali wa chama,madiwani na wanachama. 

(Picha na Mwamvua Mwinyi)
....
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MWENYEKITI  mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Bagamoyo ,alhaj Abdul Sharif ,anatarajia kuunda baraza la wazee makada la wilaya ambapo pia ameagiza kila kata kuhakikisha zinaunda mabaraza hayo ambayo yatasaidia kushauri chama.
Aidha amesema wanajenga ofisi ndogo ya chama katika kata ya Mandela ambayo itarahisisha kufanya shughuli za chama upande wa Chalinze ili kuwepo na ofisi pande zote Chalinze na Bagamoyo.
Alhaj Sharif,alisema atahakikisha pia anaunda kamati ya uchumi ya wilaya itakayohusika kusimamia na kushughulikia masuala ya miradi na mali za chama.
Akizungumza na baadhi ya viongozi wa chama  hicho kutoka kata mbalimbali,wilaya ,madiwani ,Lugoba huko Chalinze, alisema wazee ni hazina ya chama hivyo ni vyema kuchota busara na hekima zao.
Alisema wazee wasiachwe ,wasipotezwe kwani endapo watatumiwa ni washauri wakubwa ,wa kipi kifanyike,na wapi parekebishwe .
“Mnapotembea wekeni kichwani mwenu  agenda ya kuunda baraza la wazee kwenye kata zenu,enzi za waasisi wetu walitumika sana wazee katika ushauri kwenye chama,hivyo tuendelee kuwaheshimu na kuwakimbilia kufuata hekima na busara zao”alisema alhaj Sharif.
Pamoja na hilo ,ofisi yake imefikishiwa taarifa kutoka kata ya Mandela na Msata wakisema wanayo maeneo ya kujenga ofisi ndogo ya chama na maeneo mengine.
Alhaj Sharif ,alisema maeneo yote yanafaa lakini ofisi hiyo ataijenga kata ya Mandela jimbo la Chalinze na ameshapata mabati 72 na mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amehamasika atatoa matofali 1,000 ya kuanzia ujenzi.
“Wadau wameanza kujitokeza kuhusiana na ujenzi huo ,na ninaimani tutaijenga na tutaimaliza kwa mustakabali wa chama chetu ambayo itamrahisishia katibu wa CCM Bagamoyo,kufanya majukumu yake vizuri katika pande zote”alisema alhaj Sharif.


Alhaj Sharif alisema,CCM kata zote zinapaswa kuwa na mali za chama ,hivyo kama wana maeneo ya chama ni vyema yakatumika kufanya shughuli za kuzalisha kwa maslahi ya chama na kujiongezea mapato.


Hata hivyo alielezea kuwa, ana kazi katika safari yake ya uongozi kufufua mali zilizokuwa zimekufa na kuanzisha vitega uchumi na kujenga na kukarabati ofisi za chama pale penye mahitaji hayo.
Mwenyekiti huyo ,aliomba ushirikiano kwa wanachama,viongozi wa CCM ngazi za chini hadi wilaya ili kukibadilisha chama kiweze kupiga hatua kimaendeleo.
Alhaj Sharif ,alisema amedhamiria kurejesha chama kwa wanachama  badala ya wanachama kufuata viongozi maofisini.
Nae mbunge wa jimbo la Chalinze,alisema atampa ushirikiano mwenyekiti huyo,hatomwacha peke yake, ili kusimamia utekelezaji wa ilani katika halmashauri katika kutatua kero na changamoto zinazowakabili wananchi kijumla.
“Simamia halmashauri zetu ili tuhuma zinazoelekezwa zishughulikiwe,Chama kisimame imara ,”kitoe ushauri na kuhakikisha halmashauri zinafanya kazi vizuri”alisema Ridhiwani.
Ridhiwani alisema ni wakati wa mwenyekiti wa Chama wa wilaya kusimamia ilani,kwani nguvu amepewa ndani ya katiba :,anauwezo wa kutembelea miradi na kujiridhisha penye mapungufu yaweze kuyafanyia kazi na mengine kuyatolea ushauri.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages