Watu watatu wafariki na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha Noah na lori - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka

Habari za Hivi Punde

Tangaza Hapa +255755300337

Post Top Ad

Post Top Ad


Wednesday, 6 September 2017

Watu watatu wafariki na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha Noah na lori

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani (ACP)Jonathan Shanna 

 (Picha na Mwamvua Mwinyi )

...
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze

WATU watatu wanaodaiwa ni wafuasi wa chama cha wananchi (CUF)ambao wametoka katika shughuli ya kuapishwa kwa wabunge wa chama hicho mjini Dodoma wamefariki dunia ,katika ajali ya gari.

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia september 6 ,maeneo ya kijiji cha Ubena Zomozi barabara ya Morogoro/Dsm , wilaya ya kipolisi chalinze mkoa wa Pwani baada ya gari waliokuwa wakisafiria aina ya Noah kugongana uso kwa uso na scania lori .


Aidha katika ajali hiyo watu wengine watatu wamejeruhiwa na wamekimbizwa kituo cha afya Chalinze ,kwa ajili ya matibabu.

Akizungumzia kuhusiana na tukio hilo ,kamanda wa polisi mkoani Pwani ,(ACP)Jonathan Shanna ,alisema magari mawili yamegongana usiku wa kuamkia leo na kusababisha vifo na majeruhi hao.

Alieleza inasemekana watu hao waliofariki walikuwa wakitokea kushangilia kuapishwa kwa baadhi ya viongozi wao Dodoma .

Kamanda Shanna anasema watu hao walikuwa kwenye,gari no T.968CSK aina ya Toyota Noah ikiendeshwa na dereva Uledi Sarumaa(32),muislam mkazi wa Muheza.

Gari hiyo iligongana na gari no.T929 CBK/T472 CAX aina ya Scania iliyokuwa ikiendeshwa na Yasin Hamad (Kanoni) mnyamwezi(35)muislam,mkazi wa Dsm.

Aliwataja waliofariki kuwa ni dereva wa Noah Uledi Sarumaa, Mary Komba mkazi wa Muheza ,na mwingine ametambulika kwa jina moja la Isack anaekadiriwa kuwa na miaka( 37).
 
Kamanda Shanna ,alisema waliojeruhiwa ni Juma Nindi (45),Chausiku Hassan na Easter Mafie (67)wote wakazi wa Muheza.

Chanzo cha ajali kinadaiwa kuwa ni uchovu ama usingizi wa dereva wa Noah ambae alihama eneo lake kwenda upande wa kulia na kugonga lori .

Kamanda Shanna ,alieleza miili ya marehemu imehifadhiwa hospitali ya rufaa ya mkoa ya Tumbi kwa kusubiri uchunguzi wa daktari .

Dereva wa lori ametoroka mara baada ya kutokea ajali na juhudi za kumtafuta zinafanyika. 

Kamanda huyo alikemea tabia ya kuovertake bila kuwa makini na kuendesha usiku wakati dereva akiwa amechoka kwani husababisha ajali .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Tangaza Hapa +255755300337