Warsha ya wadau wa majengo Kukuza mkakati wa mawasiliano wa AQRB yafanyika jijini Dar es Salaam - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka

Habari za Hivi Punde

Tangaza Hapa +255755300337

Post Top Ad

Post Top Ad


Wednesday, 13 September 2017

Warsha ya wadau wa majengo Kukuza mkakati wa mawasiliano wa AQRB yafanyika jijini Dar es Salaam

 QS Albert munuoKaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB)  akisoma taarifa wakati akifungua Warsha ya wadau wa majengo Kukuza mkakati mawasiliano wa AQRB ilioandaliwa na  UDBS  kwaniaba ya AQRB iliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Dkt, Tumsifu Elly akiwakilisha mada yake wakati wa warsha ya wadau wa majengo Kukuza mkakati mawasiliano wa AQRB ilioandaliwa na  UDBS  kwaniaba ya AQRB iliofanyika jijini Dar es Salaam.
Muhadhiri Msaidizi kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bw Abdallah Katunzi  akielezea  Malengo ya mpango mkakati wa kimawasiliano wakati wa warsha ya wadau wa majengo Kukuza mkakati mawasiliano wa AQRB ilioandaliwa na  UDBS  kwaniaba ya AQRB iliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Muhadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bi Sophia Ndimbalema akitoa kuhusina na Malengo ya mpango mkakati wa kimawasiliano. 
Mkaguzi wa ndani (AQRB), Bw Ezekiel Stephen akiwakilisha mada yake.
Mwanasheria wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Bw Ibrahimu Mohamed akielezea malengo mkakati wa mawasiliano ya Bodi hiyo.
Wadau mbalimbali wa majengo wakifuatili kwaumakini mada katika warsha ya Kukuza mkakati mawasiliano wa AQRB ilioandaliwa na  UDBS  kwaniaba ya AQRB iliofanyika jijini Dar es Salaam.
Warsha ikiendelea.
Wadau wa majengo  wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa warsha ya Kukuza mkakati mawasiliano wa AQRB ilioandaliwa na  UDBS  kwaniaba ya AQRB iliofanyika jijini Dar es Salaam.
1.0 Maelezo kuhusu Bodi

Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo Wakadiriaji Majenzi ni taasisi ya Serikali ambayo imeanzishwa kwa sheria Na. 4 ya mwaka 2010, na iko chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilano.
Majukumu ya Bodi ni pamoja na kusaji na kudhibiti mienendo ya Wabunifu Majengo, Wakadiriaji Majenzi, Wataalamu wanaoshabihiana nao na makampuni yao.

Pia kukuza uelewa na kuelimisha jamii kuhusu taaluma za Ubunifu Majengo na Ukadiriaji Majenzi ikiwemo kazi na wajibu wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi.


Lengo la mkutano ni kuwashirikisha wadau wa Bodi katika mchakato wa kuandaa mkakati wa mawasilano wa bodi, kwa kuzingatia uzoefu wao katika mada husika.

2.0  Majukumu ya Mkakati wa Mawasiliano

Jukumu la mkakati wa mawasiliano ni kuhamasisha na kushirikishana  mawasiliano kuhusu majukumu ya Bodi na wadau katika sekta ya ujenzi.

Aidha mkakati wa mawasiliano unalenga kuelemisha jamii kuhusu majukumu ya Bodi, wabunifu majengo, wakadiriaji majenzi na wataalum wanaoshabihiana nao.

Kwa sasa sehemu kubwa ya jamii haitofautishi wabunifu majengo, wakadiriaji majenzi na wahandisi; wote wanatambulika kama wahandisi Hii sio sahihi kwa sababu kila taaluma inajitegemea, ingawa wote wanafanya majukumu yao katika sekta ya ujenzi.

Matokeo yake ni jamii kutothamini umuhimu ya huduma za ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi;hali inayofanya miradi yao kutokuwa na ubora na thamani iliyokusudiwa.


Aidha mkakati wa mawasiliano utasaidia jamii kufahamu maono , mkakati, majukumu na mafanikio ya Bodi.

2.0  Mtaalamu Mshauri

Bodi imekuwa inawasiliana na wadau kwa njia mbali mbali, ikiwa ni pamoja  na semina, makongamano, tovuti, vyombo vya habari. Hata hivyo Bodi imeamua kufanyike utafiti ili kuboresha zaidi mfumo wa mawasiliano na wadau wake.

Bodi imeteua Chuo Kikuu cha Dar es Salaam- Kitengo cha Biashara kutayarisha mkakati wa mawasilaino wa Bodi ili kuhamasisha kufahamika  na wadau wake kwa Bodi katika sekta ya ujenzi.

Wadau ambao wamekaribishwa wanatoka serikali kuu, serikali za mitaa, ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, vyama vya taaluma mbali mbali, Bodi za usajil, vyuo vikuu, makampuni ya ubunifu majengo na wakadiriaji majenzi na vyombo vya habari

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Tangaza Hapa +255755300337