Wanafunzi 11638 wanatarajia kufanya mitihani ya kumaliza darasa la saba katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Tuesday, 5 September 2017

Wanafunzi 11638 wanatarajia kufanya mitihani ya kumaliza darasa la saba katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

7 wanafunzi 11638 wa darasa la saba wanatarajia kuanza kufanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ambayo itamalizika tarehe 7/9/2017.

Idadi hiyo imejumuisha wanafunzi kutoka  shule za serikali na  binafsi ambapo wasichana ni 5958 na wavulana 5680.


Akizungumza kuhusu maandalizi ya  mtihani huu Mkurugenzi amesema maandalizi yote ya msingi yapo vizuri kabisa na yamekamilika kwa wakati.

Pia alitoa  msisitizo kwa wale wote waliochaguliwa kusimamia mitihani hiyo  kuwa waaminifu na kwa kufuata sheria walizoelekezwa za usimamizi wa mitihani.Asingependa kutokee aina yoyote ya udanganyifu katika shule za Manispaa ya Ubungo.

Aidha amewatakia kila la kheri katika mtihani huu watahiniwa wote katika shule za Manispaa ya Ubungo


Nae afisa elimu ndg.Chausiku Masegenya akitoa wito kwa wazazi amesema ni vyema wazazi wakazingatia kuhakikisha watahiniwa wanawahi shuleni kwa wakati ili kuepuka usumbufu na kuwahi kupata maelekezo kwa wakati.

Aidha alisisitiza kwa wanaosimamia mitihani hiyo kuwahi kwenye vituo vyao kwa wakati ili mambo yaende kama yalivyopangwa.


Mtihani wa kumaliza darasa la saba hufanyika kila mwaka hapa nchini ikiwa ni hatua ya kuingia elimu ya sekondari.


IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages