TANZIA: Kamishna mstaafu wa operesheni wa jeshi la zimamoto na uokoaji afariki dunia mapema leo Jijini Dar es Salaam - Mtazamo News: Home
advertise here +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

TANGAZO

advertise here +255755 300 337

Thursday, September 7, 2017

TANZIA: Kamishna mstaafu wa operesheni wa jeshi la zimamoto na uokoaji afariki dunia mapema leo Jijini Dar es Salaam


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini – Thobias Andengenye

anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Kamishna wa Operesheni Mstaafu wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CF (OPS) Rogatius Peter Kipali, kilichotokea mapema leo Semptemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake Mombasa, Ukonga jijini Dar es Salaam.


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anatoa pole kwa Maafisa, Askari na

Watumishi wote wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, familia ya Marehemu na
wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna tofauti tofauti.


Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na familia ya Marehemu linaendelea

kuratibu shughuli za msiba huo na taarifa za Mazishi zitatolewa baadaye baada
ya taratibu zote kukamilika.


Mwenyezi

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi


Amina.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Post Bottom Ad


Pages