Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Jumuia ya Afrika Mashariki JAMAFEST. Lafana - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Sunday, 10 September 2017

Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Jumuia ya Afrika Mashariki JAMAFEST. Lafana

 Wasanii wa kikundi cha Kakau Band kutoka Bukoba wakitumbuiza katika jukwaa la Tanzania wakati wa mchana.
 Wasanii wa kikundi cha Taifa cha  Utamaduni cha Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar wakicheza ngoma ya Msewe ambayo ni maafuru Kisiwani Pemba.
 Watanzania wakishangilia na kucheza katika JAMAFEST aliyevaa safari suti ni
    Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uganda Bw. Elibariki Maleko.
 Wasanii wa kikundi cha Taifa cha  Wizara Habari, Utamaduni, Utalii na
    Michezo Zanzibar wakicheza ngoma ya asali ya Zanzibar.
 Aliyesimama na kushika Microphon Bw. Iddi Suwed Mkurugenzi Mkuu wa
    Kikundi cha taifa cha tarabu cha Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na
    Michezo Zanzibar wakati wakitumbuiza nchini Uganda.
 Aliyevaa suti ya bluu na skafu ya bendendera ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanania ni Kaimu Balozi  ambaye pia ni Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Bw. Elibariki Maleko, aliyevaa shati jeupe ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Tanzania Bara Profesa Elisante Ole Gabriel wa Naibu Katibu Mkuu wake Bi. Nuru Milao wakiangalia ngoma za utamaduni katika unoesho la usiku.
Baadhi ya Watanzania wakiangalia ngoma za utamaduni wakati wa onesho la sanaa usiku.
...
Tamasha la Sanaa na Tamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST limeanza rasmi jana katikati ya mji wa Kampala kwa wasanii wa sanaa za ubunifu za  ngoma za utamaduni kwa kuoneshwa bidhaa zao mbali mbali za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Katika jukwaa la Tanzania Kikundi cha Taifa cha Utamaduni cha Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo cha Zanzibar,  Jinogile Band, Kakau Band na kikundi cha Taarabu cha Taifa cha Zanzibar vilitia fora na kuwa kivutio kikubwa kwa wananchi waliofika katika Tamasha hilo.

Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki linatarajiwa kufunguliwa rami leo na Rais wa Uganda Kaguta Yoweri Museveni katika viwanja vya Kololo na kauli mbiu ya Tanasha hili ni Utamaduni na ubunifu wa viwanda ni injini ya umoja na ajira

JAMAFEST ni tamasha lenye lengo la kuwaunganisha wasanii wasanaa za ubunifu za utamaduni kwa kutafuta soko la bidhaa hiyo adimu yenye wazalishaji wengi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki  ambayo inakuza sekta ya utalii katika Jumuiya na kwa mwaka huu Tanzania imewakilishwa na washiriki zaidi ya 200.

Washiriki wa Tanzania katika maonesho ya jana kwa upande wa Tanzania yaliongozwa na Kaimu Balozi ambaye pia ni Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Bw. Elibariki Maleko, Mshauri wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wa Mambo ya Utamaduni na Utalii Mhe. Chimbeni Kheri, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Tanzania Bara Profesa Elisante Ole Gabriel wa Naibu Katibu Mkuu wake Bi. Nuru Milao pamoja na Watanzana wanaoishi na kusoma nchini Uganda.

Washiriki wa Tanzania wamekuwa na lengo la kuonesha  bidhaa ngoma za utamaduni, nguo, shanga, dawa za mitishamba, lugha ya kiswahili, vyakula, mapishi na ulimbwende.

Habari na Picha

           Wizara ya Mambo y Nje n Ushirikiano wa Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages