Rais Dkt. Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wasali katika Kanisa la Waadventista Wasabato la Magomeni jijini Dar es salaam - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Saturday, 2 September 2017

Rais Dkt. Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wasali katika Kanisa la Waadventista Wasabato la Magomeni jijini Dar es salaam

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amepiga magoti na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Waumini wengine wa Kanisa la Waadventista Wasabato Ushirika wa Magomeni Mwembechai katika Ibada ya Jumamosi kanisani hapo  jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na   mkewe Mama Janeth Magufuli wakiimba nyimbo katika ibada hiyo ya Jumamosi katika Kanisa la Waadventista Wasabato Ushirika wa Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na   mkewe Mama Janeth Magufuli wakisikiliza neno katika Ibada hiyo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisoma neno pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli kanisani hapo wakati wa Ibada ya jumamosi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amepiga magoti pamoja na  mkewe Mama Janeth Magufuli wakati wakiombewa sala  na Maaskofu wa Kanisa hilo la Waadventista Wasabato, Sala iliyokuwa ikiongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania Marc Walwa Malekana(wa kwanza kushoto)
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa la Waadventista la Wasabato Ushirika wa Magomeni Mwembechai  kabla ya kuendesha Harambee ya Ujenzi wa kanisa hilo ambapo zaidi ya Sh. 25milioni ziliahidiwa kukusanywa.
 Waumini mbalimbali wa Kanisa hilo wakiwa ibadani kama wanavyoonekana pichani. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mama Navana Cable aliyeambatana na mtoto  wake Rebecca Cable ambao familia yao imeahidi kumalizia ujenzi wa Kanisa hilo la Waadventista la Wasabato mara baada ya Rais Dkt. Magufuli kuendesha Harambee ya Papo kwa papo Kanisani hapo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mhariri Mtendaji waMagazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonaz mara baada ya kuahidi kuchangia katika kanisa hilo.
 Waziri Mstaafu katika awamu iliyopita Steven Wasira naye akichangia katika Harambee hiyo Kanisani hapo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Ndugu Dkt. Edward Hosea mara baada ya kuchangia katika ujenzi wa kanisa hilo la Wasabato lililopo Magomeni.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshika mkono mtoto ambaye alikua anamsalimia wakati akitoka ibadani katika kanisa hilo la Magomeni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakati wakikabidhi mifuko 400 ya Saruji itakayotumika katika ujenzi wa Kanisa hilo la Wasabato la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages