Matukio katika picha Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST - Mtazamo News
Tangaza Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Monday, 11 September 2017

Matukio katika picha Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST

 Mhe. Ali Kirunda Kivejinja Naibu Waziri Mkuu ambaye  ni Waziri wa Wazira ya Mambo ya Afrika Mashariki  Nchini Uganda, pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki  akifungua kongamano la Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) leo katika hoteli ya Africana jiijini Kampala nchini Uganda, aliwasisitiza Wanajumuiya ya Afrika  Mashariki kwamba madiliko ya uchumi wa Afrika yataletwa na Waafrika wenyewe kwa kupitia sanaa na utamaduni wao.
 Waliokaa mstari wa mbele ni baadhi  ya Washiriki wa Tanzania JAMAFESTI waliohudhuria uzinduzi wa Kongamano la JAMAFEST lenye kauli mbiu ya " Utamaduni na ubunifu wa viwanda ni injini ya umoja na kutengeneza ajira".
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Tanzania Bara Profesa Elisante Ole Gabriel aliyevaa skafu yenye rangi za bendera ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, akisikiliza kwa makini maelezo ya ufunguzi wa Kongamano la JAMAFEST.
 Baadhi ya Wajasiriamali na Wasanii wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakicheza ngoma ya sindimba katika Uwanja Uhuru wa Kololo ambapo yanafanyika maonesho ya bidhaa za utamaduni na sanaa.
 Baadhi ya wajasiriamali wa bidhaa za ubunifu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania walipopiga picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Tanzania Bara Profesa Elisante Ole Gabriel (katikati) mara baada ya uzinduzi wa JAMAFEST jana. 
 Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Uganda Mhe. Dkt. Ruhakana Rugunda akifungua Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST jana katika Uwanja wa Uhuru Kololo.
 Alizihimiza nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendeleza Matamasha kama JAMAFEST ambayo hutumia mara kwa mara utamaduni kama njia ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo katika jamii.
 Wananchi wa Uganda wakishirkiania na wananchi kutoka nchi nyingine za Jumuiya za Afrika Mashariki walioshiriki katika ufunguzi wa JAMAFEST jana.
 Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Uganda Mhe. Dkt. Ruhakana Rugunda aliyevaa shati la kitenge pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Tanzania Bara Profesa Elisante Ole Gabriel aliyevaa shati jeupe na skafu ya bendera ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakitembea katika Uwanja wa Uhuru Kololo jana kabla ya kufungua Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST.
Mshauri wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia mwimbaji nguli wa taarab Zanzibar Mhe. Chimbeni Kheri akiwatumbuiza Wanajumuiya ya Afrika Mashariki walifika katika ufunguzi wa JAMAFEST katika vuwanja wa Uhuru wa Kololo Kampala nchini Uganda jana jioni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages