Madaktari watoa meno 7 kutoka kwa Mtoto wa mwezi mmoja - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka

Habari za Hivi Punde

Tangaza Hapa +255755300337

Post Top Ad

Post Top Ad


Saturday, 9 September 2017

Madaktari watoa meno 7 kutoka kwa Mtoto wa mwezi mmoja

Madaktari kwenye hospitali moja iliyo jimbo la magharibi mwa Inida ya Gujarat wamefanikiwa kutoa meno saba kutoka kwa mtoto wa mwezi mmoja.
“Kwa sasa mtoto yuko sawa,” daktari ambaye alifanya upasuaji huo Meet Ramatri alisema.

Alisema kuwa upasuiji huo ulifanya kwa njia mbili. Kwanza walitoa meno manne, na baadaye matatu.

Meno ya mtoto huyo yaligundulwia siku chache baada ya kuzaliwa huku Wazazi wake walimpeleka kwa daktari wakati alipata matatizo ya kunyonya,
Baada ya kumfanyia uchunguzi dakari aligundua nyama nyeupe na kumtuma kwa daktari Ramatri”Wakati nilimfanyia uchunguzi aligundua meno saba,” Dr Ramatri aliambia BBC.

Kisha alilazimika kutoa meno hayo kwa njia ya upasuajia na Sasa mtoto huyo anaweza kunyonya,” dakatari alisema, lakini aliongeza kuwa ni vigumu kujua ikiwa upasuaji huo utatatiza ukuaji wa meno ya mtoto huyo siku za usoni

CHANZO:BBS SWAHILI

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Tangaza Hapa +255755300337