Ded Sikonge : kilimo cha korosho kuwa zao jingine la biashara. - Mtazamo News
Tangaza Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Wednesday, 6 September 2017

Ded Sikonge : kilimo cha korosho kuwa zao jingine la biashara.

Na Tiganya Vincent Sikonge

HALMASHAURI ya Wilaya ya Sikonge imesema itaanzisha kilimo cha korosho kama zao mbadala la biashara litakaloungana na lile la tumbaku ikiwa ni hatua ya kuandaa malighafi kwa ajili ya viwanda,
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Sikonge na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Simon Ngatunga wakati akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Alisema kuwa hivi sasa wameshaandika barua kwa Bodi ya Korosho nchini kwa ajili ya kupatiwa miche ya mikorosho kwa ajili ya kupanda maeneo mbalimbali wilayani humo.
Ngatunga aliongeza kuwa udongo wa Sikonge unafaa kwa ajili ya zao la Korosho jambo ambalo linatoa fursa kwa wakazi wa Sikonge kuwa zao jingine linaloweza kuwapatia fedha.

Alisisitiza kuwa zao hilo pia litasaidia kupunguza uharibifu wa misitu kwa wakulima kutotegemea tumbaku pekee kama zao la biashara.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliwaagiza Viongozi wote katika Halmashauri zote nane mkoani humo kuhakikisha wanasisitiza kilimo cha korosho,alizeti na pamba kwa wilaya ya Urambo, Igunga , Kaliua ,Nzega na Uyui.

Alisema kuwa zoezi hilo linalenga kuwa na malighafi za kutosha kwa ajili ya Kiwanda cha Nyuzi Tabora  na kuweza kuanzisha kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti.

Mwanri alisisitiza kuwa ardhi ya Tabora inakubali mazao mbalimbali na hivyo wanataka kutumia fursa hiyo ya uzuri wa ardhi kumwongezea mkulima wigo wa mapato na kwa upande mwingine kuziongezea Halmashauri mapato ya ndani.

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa amewaagiza Maafisa Ugani wote mkoani hapa  kuwahamasisha wakulima kuanza maandalizi ya kilimo cha msimu ujao ili waweze kutumia mvua za mwanzo vizuri.

Alisema kuwa mvua za mwanzo ndio zinatakazo wawezesha kuvuna mazao mengi na mazuri

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages