Alikiba kwenda kenya kutumbuiza - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Sunday, 10 September 2017

Alikiba kwenda kenya kutumbuiza

Upepo mwanana bado unaendelea kumpuliza, staa namba moja wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ baada ya mgombea anayewakilisha Muungano wa Vyama vya Upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Omolo Odinga, kudaiwa kumuita nchini humo. 

Kwa mujibu wa chanzo kisicho na chembe ya shaka, Kiba anayesumbua kwa sasa na wimbo wake wa Seduce Me, alipata mwaliko huo mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni saa chache mara baada ya Odinga kushinda kesi ya uchaguzi Katika Mahakama ya Juu aliyokuwa amemfungulia Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ambaye mambo yalimuwia mazito.

Kenyatta alitangazwa mshindi wa nafasi ya urais na Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IBEC) katika uchaguzi uliofanyika nchini humo Agosti 8, mwaka huu ambapo Odinga alifungua kesi hiyo mahakamani. Baada ya mahakama kupitia hoja za pande zote, iliufuta uchaguzi huo kwa kueleza kuwa tume ya uchaguzi haikuzingatia uadilifu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages