Waziri Ummy Amuagiza Rmo wa Rukwa Kuboresha Huduma za Afya katika Ngazi zote ili Kutekeleza Sera ya Afya - Mtazamo News-Habari Bila Mipaka
Advertise Here +255755 300 337

HEADLINES

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Saturday, 19 August 2017

Waziri Ummy Amuagiza Rmo wa Rukwa Kuboresha Huduma za Afya katika Ngazi zote ili Kutekeleza Sera ya Afya

NA WAMJW-RUKWA .
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya jamii,jinsia ,Wazeee na watoto Ummy  Mwalimu  amemuagiza Mganga mkuu wa mkoa wa rukwa kuboresha huduma za afya katika ngazi zote ili kuwasaidia wananchi wa mkoa huo kulingana na sera ya afya.
Hayo ameyasema leo wakati wa ziara yake ya kukagua huduma za Afya  katika Wilaya ya Nkasi Mkoani  Rukwa.
 Maelekezo yangu ni tujenge hospitali zetu za Wilaya kwasababu pia idadi ya watu inazidi kuongezeka hivyo zitasaidiana na zile za taasisi zisizo za kiserikali ili kutimiza sera na miongozo ya Serikali?

Aidha Waziri Ummy amemtaka Mganga Mkuu wa Mkoa kufuatilia kwa ukaribu huduma zitolewazo na  hospitali za taasisi zisizo Zakiserikali ili kuhakikisha kwamba zinafuata miongozo na sera ya Afya ya Serikali.
 Kwa upande wake Mganga mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasulu amesema kuwa kuna  changamoto mbali mbali zinazoikumba Mkoa wake zikiwemo  upungufu wa watumishi wa Afya kwani Mkoa unahitaji jumla ya watumishi 3489 lakini waliopo ni watumishi 1593 sawa na 46% huku kukiwa na upungufu wa watumishi 1895 ambayo ni sawa na 54%.

Aidha Dkt. Boniface amesema kuwa  licha ya changamoto zilizopo  ameipongeza Serikali ya awamu ya Tano kupitia Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na ushirikiano na wadau mbalimbali kwa kuwajengea vyumba vya upasuaji katika vituo tisa huku vituo sita vikiwa vinamilikiwa na Serikali jambo linalosaidia kupunguza vifo vitokanavyo na kukosa upasuaji kwa muda.

Mbali na hayo Dkt. Boniface Kasulu amempongeza Mh. Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli kwa kuwapatia magari mawili ya kubebea wagonjwa jambo ambalo limesaidia kupunguza hadha ya hospitali nyingi ikiwemo vifo vya mama wajawazito
 WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya jamii,jinsia ,Wazeee na watoto Ummy  Mwalimu akisisitiza jambo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages