Waandishi wa Habari Wapewa Semina Juu ya Maambukizi ya Malaria Jijini Dar es Salaam - Mtazamo News
Tangaza Biashara yako Hapa +255755 300 337

HABARI ZA HIVI PUNDE

Post Top Ad

Advertise Here +255755 300 337

Wednesday, 23 August 2017

Waandishi wa Habari Wapewa Semina Juu ya Maambukizi ya Malaria Jijini Dar es Salaam

 Kaimu Meneja Mpango wa Kudhibiti Malaria kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Dkt. Renatha Mandike akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina ya siku moja kuhusina na hali ya malaria Nchini.

 Kiongozi Uchunguzi na Matibabu ya Malaria Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Dkt. Sigsbert Mkude akielezea Mikoa yenye maambukizi ya malaria nchini wakati wa semina ya siku moja kuhusina na hali ya malaria Nchini iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Agosti 23, 2017
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye semina.
 Mwalimu wa Kitengo cha Udhibiti Mbu waenezao Malaria kutoka Wizara ya Afya, Dkt, Charles Dismas akielezea mada kuhusina na maambukizi ya Malaria.
 Watumishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakifuatilia mada mbalimbali kwenye semina hiyo.
 Waandishi wa habari wakiwa kwenye semina hiyo.
Kiongozi Uchunguzi na Matibabu ya Malaria Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Dkt. Sigsbert Mkude akizungumza na waandishi wa habari.

PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-MTAZAMO NEWS
..............................
Wizara ya Afya nchini imesema maambukizi ya ugonjwa wa malaria ambao umekuwa chanzo cha vifo vya watu wengi yamepungua kwa asilimia kubwa ingawa bado  unaongoza kwa vifo.

Taarifa hiyo imetolewa na Dkt. Sigsbert Mkude ambaye ni Kiongozi; Uchunguzi na Matibabu ya Malaria wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwenye semina ya waandishi wa habari iliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Semina hiyo ilikuwa na lengo la kuelezea hali ya malaria nchini tangu mwaka 2015 hadi 2020 ambapo Dkt Mkude alisema kwa kiasi kikubwa wizara imefanikiwa kushusha chini takwimu za maambukizi ambapo hivi sasa yamefikia asilimia 50.
Akielezea mpango mkakati wa wizara kupambana na maradhi hayo, Mkude alisema wameona kupungua kwa maambukizi na vifo.

Akielezea muamko wa jamii katika upimaji wa malaria, mkude alisema upimaji katika vituo vya tiba imeongezeka kwani mwaka 2015 ilikuwa asilimia 60 lakini hivi sasa ni asilimia 85.

Aliongeza kuwa katika baadhi ya mikoa wamebaini malaria siyo miongoni mwa magonjwa kumi yanayosababisha vifo ingawa ukichanganya mikoa yote bado unaongoza.

Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni ya Nyanda za Juu Kusini ya Mbeya, Iringa,Njombe, ile ya kati ambayo ni Dodoma Manyara na ya Mikoa ya nyanda za Juu Kaskazini ya Kilimanjaro na Arusha.

Kwa upande wa changamoto wanazokabiliana nazo, Dkt. Mkude aliizitaja kuwa ni uhamasishaji wa jamii kutumia vyandarua kwa matumizi lengwa badala ya kutumia kinyume chake,rasimali na usafi wa mazingira.

Changamoto za kitaalam, usugu wa dawa za viua wadudu ambapo wakibaini hazifanyi kazi ipasavyo huzibadili japo huwa gharama.

 Akielezea muamko wa jamii kupima malaria, Dkt. Mkude alisema wamefanikiwa kwani mwaka 2015 idadi ya wagonjwa waliopimwa malaria ilikuwa asilimia 60 lakini hivi sasa ni zaidi ya asilimia 86.

Akielezea matibabu ya malaria,Dkt Mkude alisema dawa ya mseto inayotumika ni ile  yenye picha ya jani na si kwamba haipo kama inavyodaiwa na baadhi ya wauzaji wa dawa.

Aidha, aliongeza kuwa kuna maboresho makubwa ya tiba yanayofanywa na wizara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad


Pages